Pata taarifa kuu
MOROCCO-MAURITANIA-USHIRIKIANO

Rabat yafutilia mbali kauli iliyozua utata kati yake na Mauritania

Morocco imeutuma ujumbe wa serikali nchiniMauritania, ambao ulijaribu "kufuta kauli iliyozua utata kati ya nchi hizo mbili" baada ya afisa mmoja kutoka Morocco kubaini kwamba Mauritania ilikua sehemu ya Morocco.

Waziri Mkuu wa Morocco Abdelilah Benkirane aliyeongoza ujumbe wa serikali ya Morocco nchini Mauritania.
Waziri Mkuu wa Morocco Abdelilah Benkirane aliyeongoza ujumbe wa serikali ya Morocco nchini Mauritania. © Fadel Senna/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Morocco iliutuma ujeumbe wa serikali nchini Mauritania Jumatano wiki hii, ujumbe ambao ulikua ukiongozwa na Waziri mkuu, Abdelilah Benkirane, ili kufuta kauli ambayo ingeliweza kuleta athari kwenye mahusiano bora kati ya nchi hizi mbili," ilisema taarifa kutoka kasri ya Mfalme.

Desemba 24, Hamid Chabat, katibu mkuu wa Istiqlal, chama cha kihistoria kinachodai kutetea uhuru wa Morocco, alisema kuwa Mauritania ilikua "sehemu ya nchi ya Morocco."

Katika mkutano huo wa chama chake, Jumamosi, Desemba 24, Hamid Chabat alisema kuwa "Mauritania ilikuwa moja ya sehemu za nchi ya Morocco na ukubwa wa Morocco ulikua unaanzia katika eneo la Ceuta hadi kwenye Mto wa Senegal River."

Kauli hii ya hamid Chabat ililaaniwa na vyama vya siasa karibu vyote nchini Mauritania.

Ujumbe wa serikali ya Morocco ulipokelewa katika mji wa Zouerate kaskazini mwa nchi, na Rais Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz, Shirika la habari la serikali ya Mauritania (AMI) limearifu.

"Kauli ya Bw Chabat inamhusu mwenyewe. Si kauli ya Mfalme Mohammed, wala serikali, wala wananchi wa Morocco," alisema Bw Benkirane, akinukuliwa na shirika la habari la serikali ya Mauritania la AMI, katika taarifa fupi kwa Kiarabu baada ya kukutana kwa mazungumzo na rais Ould Abdel Aziz.

"Mahusiano yetu yanajengwa katika misingi imara ya kuheshimiana, ujirani mwema na ushirikiano wa pamoja, " Bw Benkirane alisema.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kasri la Mfalme, Mohammed VI tayari alizungumza kwa simu Jumanne wiki hii na Mohamed Ould Abdel Aziz na alibaini kwamba "anaunga mkono mahusiano ya ujirani mwema na mshikamano kati ya nchi hizo mbili."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.