Pata taarifa kuu
UN-MISAADA

UN yaomba dunia kuchanga dola bilioni 22.2 kwaajili ya misaada ya kibinadamu 2017

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa dunia kukusanya kiasi cha dola za marekani bilioni 22.2 ili kutoa misaada mwaka 2017 kwa maelfu ya raia wanaokabiliwa na vita pamoja na majanga.

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon.
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon. UN Photo/Amanda Voisard
Matangazo ya kibiashara

Mkuu waTume ya inayoshughulikia maswala ya Kibinadamu katika Umoja huo Stephen O'Brien anasema fedha hizo zinahitajika kusaidia kutatua majanga mbalimbali mwaka ujao.

Aidha ameongeza kuwa uhitaji ni mkubwa na watu wengi katika nchi zinazoshuhudia machafuko kama Syria wanahitaji misaada ya kibinadamu kama chakula, maji safi na makaazi.

Huu ndio uhitaji mkubwa wa kibinadamu tangu kumalizika kwa vita vya pili vya dunia.

Kuelekea mwaka ujao, watu Milioni 129 kote duniani wanahitaji msaada kutoka mataifa zaidi ya 30 yanayoshuhudia mizozo.

Umoja wa Mataifa unasema watu wanaohitaji msaada wa haraka ni kutoka Syria, Yemen na Afganistan.

Pamoja na Mataifa hayo, nchi ya Sudan Kusini ambayo imekuwa kwenye vita tangu mwaka 2013 inahitaji Dola za Marekani 2.5 kuwasaidia amaelfu ya wakimbizi ambao wameyakimbia makwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.