Pata taarifa kuu
Madagascar

Mkutano wa Francophonie waanza nchini Madagascar

Mkutano wa 16 unaozileta pamoja nchini zinazozungumza Kifaransa unaofahamika kama La Francophonie, unaanza siku ya Jumanne nchini Madagascar.

Kiongozi wa Francophonie Michaëlle Jean
Kiongozi wa Francophonie Michaëlle Jean Francophonie
Matangazo ya kibiashara

Wawakilishi kutoka Mataifa 57 yanayozungumza lugha hii pamoja na taasisi mbalimbali, wanakutana kujadili maswala mbalimbali yanayokumba nchi hizo.

Mkutano huu unaofanyika jijini Antananarivo unatarajiwa kumalizika tarehe 27 mwezi huu.

Huu ni mkutano wa kwanza chini ya uongozi mpya wa Michaëlle Jean raia wa Canada, ambaye amekuwa mwanamke wa kwanza kuongoza muungano wa nchi hizi.

Miongoni mwa maswala yatakayojadiliwa katika mkutano huu ni pamoja na yale ya kiuchumi, usalama na kisiasa katika nchi wanachama lakini pia dunia nzima ikiwemo ushindi wa rais mteule wa Marekani Donald Trump.

Nchi wanachama wa Francophonie: Albania, Andorra, Armenia, Ubelgiji, Benin, Bulgaria, Burkina Faso, Burundi, Cambodia, Cameroon, Canada, Canada-New-Brunswick, Canada-Quebec, Cape Verde, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Comoros, Congo, Cyprus, DRC, Congo, Djibouti, Dominica, Egypt, Equatorial Guinea, France, Gabon, Ghana, Greece.

Mengine ni pamoja na:- Guinea, Guinea-Bissau, Haiti, Ivory Coast, Laos, Lebanon, Luxembourg, Macedonia, Madagascar, Mali, Morocco, Mauritius, Mauritania, Moldova, Monaco, Niger, Qatar, Romania, Rwanda, Saint Lucia, Säo Tomé and Principe, Senegal, Ushelisheli, Switzerland, Togo, Tunisia, Vanuatu, Vietnam.

Waangalizi mataifa 23:- Austria, Bosnia and Herzegovina, Costa Rica, Croatia, Czech Republic, Dominican Republic, Estonia, Georgia, Hungary, Kosovo, Latvia, Lithuania, Mexico, Montenegro, Mozambique, Poland, Serbia, Slovakia, Slovenia, Thailand, Ukraine, Mmiliki za Kiarabu na Uruguay.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.