Pata taarifa kuu
TUNISIA-SIASA-HAKI

Waathirika wa Ben Ali wazungumzia hadharani masaibu yaliyowakuta

Kwa mara ya kwanza tangu rais Ben Ali kupinduliwa madarakani mwaka 2011, waathirika wa ukandamizaji uliyoendeshwa na utawala wake wataanza kusikilizwa kuanzia Alhamisi hiikwenye televisheni na redio ya taifa.

Raia wa Tunisia washerehekea maadhimisho ya mwaka mmoja wa mapinduzi yaliyomutimua mamlakani Ben Ali Februari 14, 2011 katika mtaa wa Habib Bourguiba mjini Tunis.
Raia wa Tunisia washerehekea maadhimisho ya mwaka mmoja wa mapinduzi yaliyomutimua mamlakani Ben Ali Februari 14, 2011 katika mtaa wa Habib Bourguiba mjini Tunis. AFP PHOTO/FETHI BELAID
Matangazo ya kibiashara

Kwa siku mbili, watu zaidi ya thelathini waliokua wakilalamika kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu watatoa ushahidi mbele ya wananchi wa Tunisia.

Zoezi hili litakalorushwa moja kwa moja kwenye televisheni na redio ya taifa, ni hatua muhimu kwa kazi iliyokabidhiwa Tume ya Ukweli na Maridhiano (IVD), iliyoundwa miaka miwili iliyopita ili kuorodhesha malalamiko ya waathirika wa ukiukwaji uliyotekelezwa wakati wa utawala wa Ben Ali, tangu mwaka 1987 hadi mwaka 2011.

Malalamiko 65 000 yaliwasilishwa kwa mahakama mbalimbali nchini Tunisia.

"Kwa sasa, tumewahoji kwa faragha watu 7000. Kusikilizwa hadharani ni fursa ya kupeana taarifa na jamii kuhusu maovu yaliyotekelezwa katika utawala uliyopita na kujifunza jinsi ya kuepukana nayo," amesema Sihem Bensedrine Mwenyekiti wa Tume ya Ukweli na Maridhiano (IVD).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.