Pata taarifa kuu
UGANDA-UNHRC

Uganda: Hatulindi vitendo ubaguzi wa kijinsia, ila hatuungi mkono ushoga

Nchi ya Uganda imeiambia tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa kuwa "haina uvumilivu" kuhusu ubaguzi hasa linapokuja saula la jinsia, tuhuma ambayo ilikuwa imeelekezwa moja kwa moja kwa Serikali ya Uganda, kuwa inakiuka haki za watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja. 

Picha ikimuonesha mwanaume aliyevalia mavazi ya kike, ushoga ni kosa la jinai kwenye nchi nyingi za Afrika.
Picha ikimuonesha mwanaume aliyevalia mavazi ya kike, ushoga ni kosa la jinai kwenye nchi nyingi za Afrika. REUTERS/Tyrone Siu
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Uganda, Sam Kutesa, pia ameilaumu nchi ya Uingereza kwa kile alichosema sheria zake za kikoloni ambazo bado zimesalia kwenye katiba ya nchi yao, zinakataza ushoga.

"Hatukubali na wala hatuna uvumilivu wa vitendo vyovyote vya ubaguzi wa jinsi," alisema waziri Kutesa.

Kutesa alikuwa akizungumza haya wakati wa mkutano wa kila mwaka wa tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa, kama sehemu ya utamaduni wake wa kupitia ripoti ya haki za binadamu kwa nchi wanachama, na mara ya mwisho nchi ya Uganda ilitathminiwa mwaka 2011.

Toka wakati huo, wabunge nchini Uganda, wamepitisha miswada ya sheria ambayo inataka kutolewa kwa adhabu ya kifo kwa mtu au watu watakaopatikana wakishiriki vitendo vya mapanzi ya jinsia moja, sheria ambayo ilitiwa saini na Rais Yoweri Museveni.

Mwezi Agosti mwaka huu Serikali kali ilisema kuwa mtu yeyote atakayepigwa wakati akishiriki sherehe za watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, atakuwa amejitakia mwenyewe.

Waziri Kutesa ameliambia baraza la tume ya haki za binadamu kuwa, haiko tayari kuhuburi haki za mashiga, lakini akasisitiza kuwa Serikali haikusiki pia na kutungwa kwa sheria kali inayokataza ushoga.

Wakati wa mkutano huu, nchi kadhaa za Ulaya pamoja na zile za Amerika na Latin Amerika zilitoa wito kwa nchi ya Uganda kuachana na sheria kali dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.