Pata taarifa kuu
IFJ-CPJ-RSF-VYOMBO VYA HABARI

IFJ: maandalizi na ulinzi wa waandishi wa habari katika maeneo ya vita

Jumatano hii, Novemba 2, 2016 ni sherehe ya siku ya tatu ya Kimataifa ya kukomesha tabia ya kutoadhibu uhalifu dhidi ya waandishi wa habari. Tarehe hii ilichaguliwa katika kuwakumbuka Ghislaine Dupont na Claude Verlon, waandishi wa habari wa RFI waliouawa katika mji wa Kidal, nchini Mali mwaka 2013.

Mwandishi wa habari akiangalia simu yake ya mkononi katika eneo la vita.
Mwandishi wa habari akiangalia simu yake ya mkononi katika eneo la vita. Eddie Gerald / Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Siku hii inasherehekewa kwa heshima ya waandishi wa habari wote wanaojitolea maisha yao kwa kufanya kazi yao hii, licha ya kukabiliwa na mambo mengi hususan vita. Siku hii ni fursa ya kujiuliza jinsi waandishi wa habari hujiandaa kwa kutekeleza kazi yao katika maeneo ya migogoro, bila kujali hatari inayowakabili.

Uhamasishaji wa kupata na kuwashitaki wale waliohusika kwa mauaji ya waandishi wa habari wa RFI, Ghislaine Dupont na Claude Verlon, ni swali la mazoezi ya uandishi wa habari katika maeneo ya migogoro na vita. "Tangu miaka ya 1980, kumeshuhudiwa matukio mawili, " amesema Aimé-Jules Bizimana, muhadhiri wa Chuo Kikuu cha Québec na mtaalamu katika uandishi wa habari wa masuala ya kivita. "Kwa upande mmoja, msimamo mkali wa baadhi ya makundi ya watu, ambao hawataki mabaya yao yazungumziwe. Waandishi wa habari ni mashahidi wasumbufu kwa watu hao. Aidha, kwa upande mwengine, kupitia malipo ya fidia, utekaji nyara wa waandishi wa habari umekuwa chanzo cha mapato, na hivyo kuongezeka kwa visa vya utekaji nyara kwa waandishi wa habari . Kwa uhakika, waandishi wa habari wamekua sasa wakilengwa katika migogoro mbalimbali. "

Vigezo hatari

Kama ilivyoelezwa na Shirika la Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ), nchi ambapo waandishi wa habari wako hatarini zaidi, na ambapo uhalifu unaowalenga hauadhibiwi, ni zile zinazokabiliwa na vita, migogoro, au ziko chini ya utawala wa kimabavu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.