Pata taarifa kuu
DRC-FDLR-USALAMA

Kiongozi wa waasi wa Rwanda akamatwa mashariki mwa DRC

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) limetangaza Jumatatu hii kwamba limemkamata kiongozi wa waasi wa Kihutu wa Rwanda (FDLR) mashariki mwa DR Congo. Kundi hili la waasi wa Rwanda linashtumiwa kuhusika na visa vingi vya mauaji katika ardhi ya DR Congo.

Kundi la wapiganaji wa FDLR, nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (picha ya zamani).
Kundi la wapiganaji wa FDLR, nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (picha ya zamani). Reuters
Matangazo ya kibiashara

Majeshi ya DRC (FARDC) "yalimkamata afisa mwandamizi wa kundi la waasi la FDLR katika mji wa Rutshuru" katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Meja Guillaume Ndjike, mmoja wa wasemaji wa jeshi katika mkoa huo, ameliambia shirika la habari la AFP.

Kanali Habyarimana Mucebo Sofuni mkuu wa upelelezi katika uongozi wa kundi la wasi wa Rwanda la FDLR, mashariki mwa DRC, amekamatwa Jumapili katika eneo la Kiwanja, shirika lisilo la kiserikali la Cepadho, lenye makao yake makuu mkoani Kivu Kaskazini, limearifu

Kiwanja ni kijiji kilio kwenye umbali wa kilomita 75 kaskazini mwa mji wa Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini.

Kiongozi wa waasi 'amesafirishwa mjini Goma ili aweze kuhojiwa, 'amesema Meja Ndjike, bila hata hivyo kutoa maelezo ya mazingira ambamo alikamatwa.

Kundi la waasi la FDLR liliundwa na wakimbizi wa Kihutu wa Rwanda mashariki mwa DRC baada ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, mauaji ambayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 800,000 kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Kundi hili linapingwa na utawala wa Kigali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.