Pata taarifa kuu
MAURITANIA

Rais wa Mauritania asema hana nia ya kuwania urais kwa muhula wa tatu

Rais wa Mauritania, Mohammed Ould Abdel Aziz, amesema kuwa mihula miwili ya kukaa madarakani kwa rais itaendelea kusalia kama ilivyo, kauli anayoitoa baada ya miezi kadhaa ya uvumi kuwa huenda akajaribu kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Rais wa Mauritania, Mohammed Ould Abdel Aziz
Rais wa Mauritania, Mohammed Ould Abdel Aziz REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza wakati akifunga kongamano lililowakutanisha viongozi wa vyama vya siasa nchini humo, Rais Abdel Azizi, amesema kuwa mjadala kuhusu pendekezo la kuongezwa kwa mihula ya rais kuwa madarakani, unafungwa rasmi.

Mohammed Ould Abdel Aziz amewataka wanasiasa nchini humo kuachana kabisa na mjadala kuhusu mihula ya rais kuwa madarakani, na badala yake akasisitiza kuwa mihula itasilia kuwa miwili pekee na haitabadilika.

Rais Aziz aliingia madarakani mwaka 2008 kwa mapinduzi, kabla ya kuchaguliwa mwaka 2009 na kuchaguliwa tena mwaka 2014, amesema ataheshimu muda wa mihula miwili uliowekwa kikatiba, na kwamba kwa namna yoyote ile hatajaribu kubadilisha kipengele hicho.

Msisitizo huu ameutoa hata wakati huu ambapo wafuasi wake katika siasa wakimshauri kuwa anaweza kuwania kwa muhula mwingine ikiwa wananchi watapiga kura kukubali kufanyika mabadiliko ya katiba kurekebisha kipengele hicho.

Nchi nyingi barani Afrika, hususani katika ukanda wa Afrika Mashariki zimeshafanyia mabadiliko katiba zao na kuongeza mihula ya rais na wengine kutokuwa na ukomo wa rais kuwa madarakani, hali inayosababisha vurugu kama ambazo zinashuhudiwa nchini DRC.

Rais Abdel Aziz ameongeza kuwa hata kipengele cha umri wa rais kukaa madarakani hakitabadilishwa na kitasalia kama kilivyo hivi sasa.

Matamshi yake tayari yamepongezwa na wanaharakati wa demokrasia nchini humo, ambao wanasema rais wao ameonesha ukomavu wa kisiasa kwa kukubali kuheshimu katiba ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.