Pata taarifa kuu
TUNISIA-USALAMA

Uingereza yapeleka wataalamu kutoa mafunzo ya kijeshi Tunisia

Uingereza imepeleka maafisa arobaini wa kijeshi nchini Tunisia kutoa mafunzo ya kijeshi kwa lengo la kuisaidia nchi hiyo ya Afrika kaskazini kuzuia kusambaa kwa wapiganaji wa Islamic State kutoka taifa jirani la Libya,wizara ya ulinzi ya Uingereza imefahamisha.

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza  Michael Fallon
Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Michael Fallon REUTERS/Hadi Mizban/Pool
Matangazo ya kibiashara

Mafunzo hayo yatakuwa katika kuimarisha oparesheni za kiintelijensia,ukaguzi na doria,huu ni mpango wa tatu kufanywa na jeshi la uingereza nchini Tunisia tangu waingereza 30 kuuawa katika shambulizi la ufukweni nchini Tunisia.

Mauaji ya June mwaka jana katika hoteli ya Sousse huko pwani ya Mediterania lilikuwa pigo kubwa kwa Uingereza kando na lile la London julai 2005.

Waziri wa ulinzi wa Uingereza Michael Fallon amesema uingereza imejipanga kuisaidia Tunisia ambayo ni mshirika wake katika mapambano dhidi ya kundi la Daesh ama islamic state ambalo liliteketeza maisha ya waingereza wasiokuwa na hatia katika shambulizi la mwaka jana.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.