Pata taarifa kuu
DRC -USALAMA

Kiongozi wa waasi DRC ajisalimisha

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kiongozi wa kivita ambaye alikua bado hajapatikana tangu kutoroka kwake kutoka gerezani mwaka 2011 alijisalimisha kwa viongozi wa mkoa wa Lubumbashi Jumanne wiki hii, kusini mwa nchi hiyo.

Gédéon Kyungu alijisalimisha kwa viongozi mjini Lubumbashi wakati wa sherehe, Jumanne, Oktoba 11, 2016.
Gédéon Kyungu alijisalimisha kwa viongozi mjini Lubumbashi wakati wa sherehe, Jumanne, Oktoba 11, 2016. Radio Okapi
Matangazo ya kibiashara

Gédéon Kyungu alikua akionogza kundi la waasi la 'Bakata Katanga', wanamgambo ambao jina lake katika Kiswahili sanifu linamaanisha "kuigawa Katanga", mkoa wa kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Pamoja na watu wake, Bw Kyungu alikua akiendesha harakati zake kusini mwa nchi, ambapo makundi ya wanamgambo walishambulia raia na kuwapora mali zao na rasilimali za madini.

Gédéon Kyungu alikuwa alikamatwa na kuhukumiwa mwaka 2009 mjini Lubumbashi, mji wa pili wa nchi hiyo, kufuatia hukumu kwa uhalifu dhidi ya binadamu.

Akiwa mafichoni tangu mwaka 2011, Bw Kyungu alionekana mbele ya viongozi mjini Lubumbashi, pamoja na baadhi ya wapiganaji 100 wakati wa sherehe ya kujisalimisha iliyofanyika Jumanne wiki hii katika kijiji cha Malambwe, kwa mujibu wa Gavana wa mkoa wa Haut-Katanga, Jean-Claude Kazembe.

"Nimekuja ili kutekeleza wito wa rais ambaye anataka amani," Bw Kyungu.

Kiongozi huyo wa kivita alionekana mdhaifu, huku akivaa fulana yenye picha ya Rais Joseph Kabila, wakati wa sherehe za kujisalimisha.

Bw Kazembe alisema anaamini kuwa Gedeon Kyungu amejisalimisha ili kufaidika na mpango wa kuwarejesha waasi katika maisa ya kiraia.

Serikali ya DR Congo imekua ikikosoa na mashirika ya haki za binadamu kwa mpango huu wa kuunganisha wapiganaji katika jeshi la taifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.