Pata taarifa kuu
DRC

Watu 13 wapoteza maisha baada ya kukanyagana mjini Beni nchini DRC

Wakaazi wa mji wa Beni Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanaomboleza vifo vya watu 13 waliopoteza maisha baada ya kukanyagana.

Barabara kuu ya mji wa Beni Mashariki mwa DRC
Barabara kuu ya mji wa Beni Mashariki mwa DRC Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lilijiri siku ya Jumamosi  baada ya mwanajeshi wa serikali aliyekuwa mlevi kufwatua risasi hewani na kuzua hali ya wasiwasi katika mji huo.

Meya wa mji huo Jean Edmond Nyonyi, amesema mwanajeshi huyo alikuwa hajavalia sare wakati alipotekeleza  kitendo hicho na kusababisha watu wengine nane kuzama mtoni baada ya kukumbwa na wasiwasi kuwa walikuwa wanalengwa.

Wakaazi wa mji wa Beni wamekuwa wakiishi kwa hofu kwa muda mrefu  kwa sababu za kiusalama baada ya watu zaidi ya 50 kuuawa mwezi uliopita mikononi mwa waasi.

Tangu mwaka 2014, watu zaidi ya 700 wamepoteza maisha baada ya kuuliwa na waasi wa ADF Nalu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.