Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-ZIDA

Burkina Faso: Rais Kaboré aamuru Isaac Zida afuatiliwe

Nchini Burkina Faso, Rais Roch Marc Christian Kaboré ameamuru vyombo husika kumfuatilia Yacouba Isaac Zida, Waziri Mkuu wa zamani katika kipindi cha mpito, ambaye kwa sasa anaishi nchini Canada. Sababu ya hatua hii: "kutoroka jeshi wakati wa amani."

Rais mpya wa Burkina Faso, Roch Marc Christian Kaboré.
Rais mpya wa Burkina Faso, Roch Marc Christian Kaboré. REUTERS/Joe Penney/Files
Matangazo ya kibiashara

Rais Roch Marc Christian Kaboré, pia Waziri wa Ulinzi wa Taifa ameagiza vyombo husika kumfuatilia jenerali Yacouba Isaac Zida kwa kosa la "utoro wakati wa amani na kukataa kutii amri." uamuzi huu ulichukuliwa Jumanne iliyopita, Septemba 13, lakini umewekwa wazi Alhamisi hii na gazeti la kila siku linalorusha habari hewani la Fasozine.

Waziri Mkuu wa zamani, ambaye, baada ya kuhudumu kwenye wadhifa huo katika serikali ya mpito, aliteuliwa kuwa afisa wa juu katika jeshi mwenye cheo cha jenerali, aliomba ruhusa ya kusafiri kwenda Canada karibu na familia yake. Ruhusa hiyo ilimaliza muda wake tangu Februari 19, 2016, na tangu wakati huo hajarejea nchini licha ya maagizo mbalimbali ya Rais Roch Marc Christian Kaboré.

JENERALI yaacouba Isaac Zida, ambaye alitajwa katika madai kadhaa ya ubadhirifu wa fedha katika Ofisi ya rais wa Burkina Faso na katika wizara mbalimbali, viongozi wa sasa walimuomba mara kadhaa jenerali Yacouba Isaac Zida kurudi nyumbani ili kutoa maelezo.

Ruhusa ya jenerali Yacouba Isaac Zida ilisainiwa na Waziri wa Ulinzi, ambaye pia ni rais wa jamhuri, Roch Marc Christian Kaboré. Na hivyo ni waziri wa ulinzi kubainisha utoro katika jeshi na kuamuru taratibu za kinidhamu. Mwezi Juni, Rais Kaboré alitishia kumchukulia jenerali Yacouba Isaac Zida kama afisa mtoro wakati wa amani, na pia alitishia kuanzisha utaratibu wa kisheria dhidi yake, kama itahitajika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.