Pata taarifa kuu
WHO-ANGOLA-DRC

WHO yatangaza kudhibitiwa kwa homa ya Manjano nchini DRC na Angola

Shirika la afya duniani WHO limetangaza kudhibitiwa kwa mlipuko wa homa ya manjano nchini Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Watoto wakipewa chanjo jijini Kinshasa nchini DRC
Watoto wakipewa chanjo jijini Kinshasa nchini DRC sciencemag.org
Matangazo ya kibiashara

WHO imetoa tangazo hilo baada ya kufanikisha chanjo kwa Mamilioni ya raia wa nchi hizo mbili katika miezi ya hivi karibuni.

Mlipuko wa ugonjwa huu ulisababisha maambukizi zaidi ya watu 4,000 tangu mwezi Desemba mwaka uliopita katika nchi hizo.

Sylvie Briand, anayeongoza idara ya magonjwa ya mlipuko amesema tishio la maambukizi ya homa hiyo sasa halipo tena.

Jiji kuu la Luanda na Kinshasa ndio maeneo yaliyoathiriwa zaidi.

WHO inasema tangu mwezi Juni mwaka huu, hakuna kisa chochote cha homa ya majano kilichoripotiwa nchini Angola sawa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tangu mwezi Julai.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.