Pata taarifa kuu
UNICEF-WATOTO

Watoto milioni hamsini waishi ukimbizini duniani kote

Umaskini na vurugu vimesababisha mamilioni ya watoto kuyatoroka makazi yao. Mara nyingi wanaishi katika mazingira magumu katika maeneo nchi wanakopewa hifadhi. Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Watoto (Unicef) inalaani ukosefu wa upatikanaji wa huduma muhimu kwa watoto hawa.

Watoto wa Eritrea wakizuliwa katika kituo wanakokusanywa wahamiaji haramu mjini Tripoli, Libya, mwezi Julai 2016.
Watoto wa Eritrea wakizuliwa katika kituo wanakokusanywa wahamiaji haramu mjini Tripoli, Libya, mwezi Julai 2016. AFP
Matangazo ya kibiashara

Karibu milioni 50 ya watoto duniani kote wanaishi "katika mazingira magumu", baada ya kulazimishwa kuhama makazi yao au nchi zao kwa sababu ya vita, vurugu na mateso, shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Watoto (Unicef) limeelezea wasiwasi wake.

Ripoti hiyo, ambayo ni mgogoro mkubwa zaidi kwa watoto wakimbizi na wahamiaji, iliyotolewa Jumatano hii na shirika la Umoja wa Mataifa, inaonyesha picha ya hali ya watoto wanaolazimishwa kuondoka katika nafasi zao za maisha.

Mwishoni mwa 2015, watu wapatao milioni 31 kati yao walikuwa wakimbizi na milioni 17 walikuwa wakimbizi wa ndani katika nchi zao.

Haja ya misaada ya kibinadamu

"Kila picha, kila kijana na kila msichana inaashiria mamilioni ya watoto wanaokabiliwa na hali ya hatari na tunahitaji huruma kwa waathirika ambao tunaona wanaishi katika mazingira kama watoto hawa", taarifa ya Unicef imesema.

Miongoni mwa watoto hawa milioni 50, milioni 28 waliyahama makazi yao kutokana na migogoro mbalimbali, na wahamiaji wa ndani na wale waliolazimika kukimbilia katika nchi za kigeni.

Hata hivyo, takriban watoto milioni 20 walilazimika kuyahama makazi yao kutokana na sababu mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.