Pata taarifa kuu
AU-GABON

AU kupatanisha pande hasimu Gabon

Nchini Gabon, hakuna vurugu kubwa zilizojitokeza katika saa za hivi karibuni, lakini bado mvutano unaendelea. Kila upande aumekua ukichukua msimamo wake baada ya kuchaguliwa kwa mara nyingine Ali Bongo katika uchaguzi wa urais.

Rais wa Chad Idriss Deby (hapa katika mkutano wa G20, Hangzhou, Septemba 4, 2016) alipendekeza kutuma ujumbe wa AU nchini Gabon.
Rais wa Chad Idriss Deby (hapa katika mkutano wa G20, Hangzhou, Septemba 4, 2016) alipendekeza kutuma ujumbe wa AU nchini Gabon. REUTERS/Mark Schiefelbein/Pool
Matangazo ya kibiashara

Katika hali ya kujaribu kutatua hali hiyo, Umoja wa Afrika umesema uko tayari kutuma ujumbe wake nchini Gabon.

Jitihada hiyo ilitangazwa katika taarifa Rais wa Chad, Idriss Déby Itno, Mwenyekiti wa sasa wa taasisi hiyo barani Afrika.Rais Idriss Deby anataka kutuma ujumbe wa viongozi wa Afrika na wawakilishi wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa "kwa haraka kama mazingira ya ziara hiyo yatakaa sawa."

Msemaji wa serikali ya Gabon, Alain-Claude bile Bi Nze, amesema wanakubaliana na pendekezo hili, "Rais Ali Bongo anakubali kuwasili kwa ujumbe huo mjini Libreville hasa kwa vile tu Rais Ali Bongoana ushahidi halali ambao ataonyesha. Na katika mila za kiafrika, si vizuri kumkatalia mtu anapoomba kukutembelea. Anatarajia kuwa ujumbe huo utakuja kutoa mchango wake ili kurejesha hali utulivu. Mategemeo yetu ni kwamba sauti ya Gabon itasikilizwa na sauti ya uhalali wa kikatiba itasikilizwa na kuheshimiwa. "

Kwa upande wa upinzani, hawakatai jitihada za Umoja wa Afrika (AU). "Kama lengo ni kumuelewesha Ali Bongo akubali matokeo ya uchaguzi, itakuwa bora kwa nchi yetu, amesema Jean-Gaspard Ntoutoume Ayi, msemaji wa kambi ya Jean Ping. Tunaangalia kwa matumaini makubwa kuwasili kwa ujumbe huo. Kama ni upatanishi, ujumbe huo utakuwa na wajibu wa kuomba kuheshimu kura za raia wa Gabon. "

Kwa kusubiri ujumbe wa Umoja wa Afrika, nini kitatokea? suala la kukata rufaa kwa Mahakama ya Katiba limejitokeza. Tarehe ya mwisho ni Alhamisi. kambi ya Ali Bongo tayari imesema itawasilisha ombi lake, itakataa rufaa kuhusu udanganyifu katika baadhi ya vituo vya kupigia kura. upande wa upinzani, kambi ya Jean Ping imeomba kwanza kabisa kurejelea zoezi la uhesabuji wa kadi za kupigia kura pamoja na mkutano mpya wa Tume ya Uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.