Pata taarifa kuu
GUINEA

Rais Alpha Conde akutana kwa mazungumzo na kiongozi wa upinzani Cellou Diallo

Rais wa Guinea Alpha Conde na kiongozi wa upinzani Cellou Dalein Diallo, wamekutana kwa mazungumzo hapo jana, ikiwa ni majuma mawili yamepita toka kushuhudiwa kwa maandamano yaliyokuwa ya vurugu, waandamanaji wakiituhumu Serikali kwa kukithiri kwa vitendo vya rushwa.

Rais wa Guinea, Alpha Conde (kulia) akipeana mkono na kiongozi wa upinzani nchini humo, Cellou Dalein Diallo, wakati walipokutana na mazungumzo, Alhamisi, September 1, 2016
Rais wa Guinea, Alpha Conde (kulia) akipeana mkono na kiongozi wa upinzani nchini humo, Cellou Dalein Diallo, wakati walipokutana na mazungumzo, Alhamisi, September 1, 2016 AFP / Cellou Binani
Matangazo ya kibiashara

Mtu mmoja alipogwa risasi na polisi huku wengine mamia wakijeruhiwa, wakati raia zaidi ya nusu milioni wa Guinea walipoandamana mjini Conakry, kupinga kile walichosema ni udhibiti mbaya wa uchumi wa taifa hilo unaofanywa na Serikali ya rais Conde.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya mazungumzo hayo, kiongozi wa upinzani Diallo, ameseme wamezungumzia masuala mengi mtambuka yanayoikabili nchi hiyo, ikiwemo hali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi, na kwamba kwenye mazungumzo yao pia walijaribu kuzungumzia tofauti zao kujaribu kuzitatua.

Kwa upande wake rais Alpha Conde amesema mazungumzo yao yaligusa maeneo mengi yanayikabili nchi hiyo, na kuongeza kuwa wamekubaliana kuendelea kukutana mara kwa mara kujaribu kumaliza tofauti zao kwa mustakabali wa taifa.

Maandamano yaliyoandaliwa na upinzani na kufanyika Agosti 17 mwaka huu, yalikuwa ni miongoni mwa ajenda zilizozungumziwa na viongozi hao, ambapo polisi wanadaiwa kuingilia maandamano ambayo yalianza kwa amani kabla ya baadae kugeuka na kuwa vurugu baada ya Polisi kuingilia kati na kuanza kuwatawanya.

Serikali imesema kuwa Polisi aliyempiga risasi hadi kufa mmoja wa waandamanaji tayari amekamatwa na atapandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kosa la mauji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.