Pata taarifa kuu
DRC - SIASA

Mazungumzo ya kitaifa yaendelea, licha ya upinzani kusisitiza msimamo wao

Mazungumzo ya kitaifa yaliyokuwa yakisubiriwa kwa muda mrefu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kujaribu kuiepusha nchi hiyo kutumbukia katika mzozo wa kisiasa, yamefunguliwa rasmi hapo jana jijini Kinshasa, licha ya kutokuwepo kwa wanasiasa muhimu wa upinzani, ambao wanasema Serikali imewatega.

Kiongozi wa chama cha UNC, Vital Kamerhe, akizungumza na wanahabari wakati wa ufunguzi wa mazungumzo ya kitaifa.
Kiongozi wa chama cha UNC, Vital Kamerhe, akizungumza na wanahabari wakati wa ufunguzi wa mazungumzo ya kitaifa. RFI / Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya muhimu kati ya Serikali na makundi ya upinzani, yanalenga kuondoa sintofahamu ya kisiasa inayoweza kujitokeza wakati muhula wa rais Josephu kabila utakapofikia tamati mwezi December mwaka huu, huku kukiwa na wasiwasi kuwa huenda akabakia madarakani.

Waandamanaji walikabiliana na Polisi nje ya ukumbi ambako mazungumzo hayo yalikuwa yanafanyika, huku mpatanishi wa umoja wa Afrika na waziri mkuu wa zamani wa Togo, Edem Kodjo, akisema ameitisha mazungumzo hayo sio kwa kufurahisha au kupendelea upande, lakini yuko kwaajili ya kuwasaidia watu wote wa DRC.

Kwenye mkutano huo, kiongozi wa upinzani aliyetengwa na muungano wa upinzani, Vital Kamerhe, amemtaka mpaanishi huyo kuahirisha mazungumzo hayo kwa siku mbili, ili yeye pamoja na wanadiplomasia wa kimataifa waende kuwashawishi wenzao kushiriki mazungumzo.

Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kuwa ikiwa Congo inataka amani ni lazima mazungumzo ya safari hii yatoke na majibu ya matatizo ya wananchi.

Mazungumzo haya yanaendelea, ambapo mpatanishi Edem Kodjo, ataeleza ikiwa wa ahirishe mazungumzo hayo ili wapate muda wa kuwashawishi wengine au yaendelee wakati ushawishi ukiendelea kando na mazungumzo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.