Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Washukiwa sita wa mauaji ya Beni wafikishwa kizimbani

Washukiwa sita wa mauaji ya mfululizo katika mkoa wa Beni Mashariki mwa DRC, wamefikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi jana Jumamosi wakati wa kusikilizwa kwa mara ya kwanza kwanza wa kesi ya mauaji hayo yanayohusishwa na waasi wa Uganda wa ADF.

Raia wakishuhudia miili ya takriban rai 51 waliuawa katika mji wa Beni mashariki mwa DRC mwezi Agosti
Raia wakishuhudia miili ya takriban rai 51 waliuawa katika mji wa Beni mashariki mwa DRC mwezi Agosti KUDRA MALIRO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Watuhumiwa hao sita ambao ni Mganda mmoja, Mtanzania mmoja na wa Kongo wanne, wamefikiswa mbele ya mahakama ya kijeshi katika mji wa Beni, amesema Kanali Jean-Paulin Esosa, wa mahakama ya jimbo la Kivu Kaskazini.

Kanali Esosa ameongeza kuwa watu hao wanashitakiwa kwa ushiriki wao katika harakati za vurugu dhidi ya serikali, uhalifu dhidi ya ubinadamu,mauaji na ugaidi katika maeneo ya Oïcha ambako walikamatwa.

Katika kesi hiyo, Watuhumiwa hao wamekiri kushirikiana na kundi la ADF, la nchini Uganda

Wananchi wengi wa mji wa Beni walijitokeza hapo jana kusikiliza kesi hiyo ambapo mmoja wa manusura wa mauaji hayo alisema angependa kuona washukiwa hao wakipewa adhabu kali ili kuwa fundisho kwa wengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.