Pata taarifa kuu
ZAMBIA-SIASA

Hichilema apinga ushindi wa rais Lungu Mahakamani

Kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema anawasilisha kesi katika Mahakama ya Kikatiba kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu yalimyompa ushindi rais Edgar Lungu.

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Zambiai UPND, Hakainde Hichildma
Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Zambiai UPND, Hakainde Hichildma REUTERS/Rogan Ward
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Uchaguzi mapema wiki hii ilimtangaza Lungu mshindi kwa kupata asilimia 50.35 ya kura zote zilizopigwa wiki iliyopita huku mpinzani wake akiwa wa pili kwa kupata asilimia 47.63 ya kura.

Wiki hii, Polisi iliwakamata zaidi ya wafuasi 150 wa upinzani katika mji wa utalii wa Livingstone Kusini mwa nchi hiyo; waliokuwa wanaandamana kupinga ushindi wa rais Lungu.

Kiongozi huyo wa upinzani anataka Mahakama hiyo kutupilia mbali matokeo hayo kwa madai ya kuwepo kwa wizi wa kura hasa jijini Lusaka.

Kuanza kwa kesi hii kutamaanisha kusitishwa kwa sherehe za kumwampisha rais Lungu zilizotarajiwa kufanyika hivi karibuni, hadi kesi hiyo itakapoamuliwa baada ya siku 14.

Wakati wa kampeni za kisiasa, Hichilema aliwaambia wafuasi wake kuwa atakwenda Mahakamani kupinga matokeo ikiwa Lungu atatangazwa mshindi, na alikuwa na uhakika wa kushinda.

Wachambuzi wa siasa nchini humo wanaonya kuwa ikiwa Mahakama itaamua kutupilia mbali matokeo hayo, wafuasi wa rais Lungu hawatakubali uamuzi huo kutokana na kauli hiyo ya Hichilema.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.