Pata taarifa kuu
DRC-BENI-MAUAJI

Serikali ya DRC yatangaza maombolezo ya kitaifa ya siku 3

Baada ya mauaji yaliyotokea Jumamosi Agosti 13, 2016, serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia msemaji wake akiwa pia Waziri wa habari, Lambert Mende imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku tatu kuanzia Jumatatu hii, baada ya mauaji ya zaidi ya watu 30 wilayani Beni, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Lambert Mende.
Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Lambert Mende. AFP PHOTO / JUNIOR D. KANNAH
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali ameeleza amesikitishwa kuona Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaendelea kukumbwa na kile alichokitaja kama tishio la wanajihadi

Lambert Mende ameyasema hayo Jumapili hii kwenye runinga ya serikali ya RTNC.

Katika taarifa iliyosomwa Jumapili hii, msemaji wa serikali ya Congo, Lambert Mende, amesema kuwa maombolezo hayo yanaanza Jumatatu, Agosti 15 na kumalizika Agosti 17.

"Nikiagizwa na Rais wa Jamhuri, serikali imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku tatu kuanzia Jumatatu 15 Agosti. bendera itapandishwa nusu mlingoti katika nchi nzima na vyombo vya habari, hususan redio na televisheni vitapeperusha matangazo ambayo yanaendana na tukio hili, " amesema Lambert Mende.

Waasi wa Uganda wa ADF wanashtumiwa kuendesha mauaji ya Jumamosi, Agosti 13, ambapo watu thelathini na sita waliuawa, katika kata ya Rwangoma, mjini Beni, katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kwa mujibu wa Waziri wa Habari, watu waliouawa ni wanaume 22 na wanawake 14.

"Kundi hili la wahalifu lilikimbia msituni baada ya kutimuliwa na vikosi vya jeshi la vya DRC viliopo katika mji wa Beni. Serikali inatoa rambirambi zake kwa familia na ndugu wa wahangabila kusahau wakazi wote wa mji Beni na katika mkoa wa Kivu Kaskazini, " amesema Mende.

Mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini Julien Paluku pia ametoa rambirambi zake kwa niaba ya serikali ya mkoa anaoongoza, akisema kusononeshwa ma mauaji ya raia kukithiri mkoni mwake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.