Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mali: mapigano yaibuka Kidal

Katika jimbo la Kidal, kaskazini mwa Mali, mapigano makali yalishuhudiwa Alhamisi Julai 21 kati ya waasi wa Tuareg na kundi la watu wenye silaha wanaounga mkono serikali ya Mali.

Wapiganaji wa kundi la waasi la Azawad (CMA) mjini Kidal Machi 28, 2016 katka mktano kwa ajili ya maridhiano.
Wapiganaji wa kundi la waasi la Azawad (CMA) mjini Kidal Machi 28, 2016 katka mktano kwa ajili ya maridhiano. AFP
Matangazo ya kibiashara

Milio ya risasi ilisikika katikati mwa mji siku chache tu baada ya kusaini mkataba wa amani. Hali ya wasiwasi imeendelea kutanda alhamisi hii jioni.

Milio ya risasi imeendelea kusikika Alhamisi mchana kutwa katika jimbo la Kidal, hata kama haihusiani na vurugu za mapigano ya mchana. Kinachojulikana tu ni kwamba karibu saa 10 jioni (saa za Mali), milio ya risasi ilizuka katikati mwa mji. Mapigano yalienea kwa karibu kila mahali na ilidumu angalau hadi saa moja usiku, wakati ambao vurugu zimepungua kwa kiasi fulani.

Baadhi ya wakazi walilazimika kubaki makwao, wengine walikimbilia katika kambi ya ya kikosi cha Umoja wa Mataifa (MINUSMA).

Ni vigumu kujua chanzo zha mapigano hayo. Upande mmoja kuna kundi la waasi la CMA, linalojumuisha makundi kadhaa ya jamii ya Watuareg, na kwa upande mwingine kuna kundi la GATIA, Kundi jingine la wapiganaji wenye silaha linalounga mkono serikali. Kila upande analaumu mwingine kuanzisha mashambulizi.

Mapigano haya hutokea wakati makataba wa kusitisha mapigano ulisainiwa Jumapili iliyopita kati ya makundi mawili. Toka Jumanne jioni, mapigano yalizuka katikati mwa mji na kusababisha vifo vya watu wawili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.