Pata taarifa kuu
DRC-LAMBERT MENDE

Serikali yalaani kuingiliwa kimataifa katika masuala ya DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, msemaji wa serikali amewanyooshea kidole cha lawama washirika wa Magharibi. Katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi hii, Julai 7, Lambert Mende aametoa maneno makali akijibu shutuma zilizoongezeka hivi karibuni.

Msemaji wa Serikali ya DRC, Lambert Mende,  akiwaambia waandishi wa habari,  Kinshasa, Aprili 13, 2015.
Msemaji wa Serikali ya DRC, Lambert Mende, akiwaambia waandishi wa habari, Kinshasa, Aprili 13, 2015. FEDERICO SCOPPA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kama kukosolewa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini humo, au vikwazo vilivyochukuliwa na Marekani dhidi ya mkuu wa polisi wa mji wa Kinshasa, Lambert Mende hakusita kusema wameanzisha tabia yao mbovu ya ukoloni, ubaguzi wa rangi na ubeberu.

"Nchi yetu, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imekua sasa ni gumzo kwa mabaya yote tunayoshtumiwa na nchi za Magharibi, ambazo zimekua zikiingilia masuala ya ndani ya nchi yetu. Rais Joseph Kabila alisema katika ujumbe wake wa Juni 30, tunakataa kuona tumekabiliwa na maporomoko ya shutma za ubeberu kutoka wale wanaojidai, ukianzia Washington hadi Brussels, pamoja na miji mingine ya nchi za magharibi, wakichukulia kisingizio cha ugumu wa tofauti zetu za ndani kuhusu mchakato wa uchaguzi wa mwaka 2016 katika nchi yetu kwa kuchochea machafuko, shutma zisizokua na msingi. Kana kwamba milioni 70 ya raia wa Congo hatuweki mbele maslahi yetu ya kitaifa, " amesema Lambert Mende.

Msemaji wa serikali pia amemshambulia Moise Katumbi,akimtaka mgombea urais kujitetea mahakamani na si katika vyombo vya habari. Lambert Mende pia amesema kuwa Mkuu wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga alikuwa anatakiwa kurudi shule, kwa sababu hajui chochote kwa utendaji kazi wa taasisi, sheria au Katiba.

Moïse Katumbi, Lubumbashi, Mei 28.
Moïse Katumbi, Lubumbashi, Mei 28. © AFP PHOTO / FEDERICO SCOPPA

Lambert Mende pia ameishukuru ofisi ya pamoja ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu kwa msaada wake kuhusu uchunguzi kuhusu ugunduzi wa miili sita ikiwa na majeraha iliyogunduliwa katika Mto Ndjili, lakini Waziri wa Mawasiliano amebaini kwamba mshirika huyo atakuwa na ufanisi zaidi kama "ataacha kudhoofisha vikosi vya usalama kwa kampeni za kushfa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.