Pata taarifa kuu
NIGER-WAHAMIAJI

Niger: wahamiaji 34 wafariki jangwani

Wahamiaji 34, ikiwa ni pamoja na watoto 20 wamekufa jangwani, karibu na kijiji cha Assamanka, kwenye eneo la mpaka kati ya Niger na Algeria. Inahofiwa kuwa watu hao walikufa kwa kiu.

Wahamiaji wa Niger katika mji wa Boufarik, Algeria 2014.
Wahamiaji wa Niger katika mji wa Boufarik, Algeria 2014. AFP PHOTO/FAROUK BATICHE
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Niger imebaini kwamba wanaume watano, wanawake tisa na hasa watoto ishirini hasa wamekufa. Katika uwezekano wote, walitelekezwa na watu waliokuwa nao, juma moaj lililopita.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Niger, watu 34 waliokutwa wamekufa nchini Niger walikuwa wakijaribu kusafiri kwenda Algeria wakipitia jangwani. "Walitelekezwa na watau waliokua wakiwasafirisha nchini Algeria" katika "wiki ya tarehe 06 hadi 12 Juni, 2016," imesema taarifa hiyo, ambayo pia imeongeza kwamba miili miwili tu ndio imetambuliwa, ikiwa ni pamoja na mwanume na mwanamke wenye umri wa miaka 26, ambao wote ni raia wa Niger.

Kwa upande wake Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema kwamba Niger ni mhimili kwa wahamiaji wanaoelekea Ulaya hasa nchini Italia, kwani 60% ya wahamiaji wanaopitia nchini Libya kwa kuingia Ulaya baada ya kuvuka bahari ya Mediterranean "wanapitia Niger." Algeria imekuwa imekua sasa njia muhimu kwa wahamiaji kutoka kusini mwa Sahara, badala ya Libya.

Katika miaka ya hivi karibuni, maelfu ya wahamiaji waingia nchini Algeria kinyume cha sheria, wengi wao wakiwa kutoka nchi jirani zinazopakana na Mali pamoja na Niger. Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Niger imeelezea "masaibu yanayowakuta wahamiaji haramu wanaojaribu kutumia nia hiyo ambapo mara nyingi wanakutana na makundi ya wahalifu".

Zaidi ya raia 7,000 kutoka Niger, ambapo nusu yao ikiwa ni wanawake na watoto, walirejeshwa makwao mwaka 2015 chini ya makubaliano kati ya Algiers na Niamey. Baada ya makubaliano yaliyotiliwa saini kati ya Umoja wa ulaya na Uturuki mwezi Machi, njia ya bahari kutoka Afrika imeanza kutumiwa kwa uficho na wahamiaji wanaoelekea Ulaya. Hata hivyo njia hiyo bado ni hatari.

Wiki iliyopita, Tume ya Ulaya iliwasilisha mpango kwa nchi za Afrika, ikipendekeza kutoa, ifikapo mwaka 2020, Euro bilioni 8 kutoka fuko la fedha zilizopo kwa misaada ya maendeleo kwa nchi ambazo zitakubali kupokea wimbi la wahamiaji, kwa minajili ya kukabiliana na tishio la "madhara" kuhusu mpango wa kibiashara kwa wengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.