Pata taarifa kuu
CAR-SERIKALI-SIASA-USALAMA

CAR: serikali mpya yatangazwa

Serikali mpya ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imetangazwa Jumatatu hii Aprili 11. Baadhi ya mawaziri wa zamani katika utawala wa François Bozizé wameteuliwa katika wizara mbalimbali.

Washirika wengi wa karibu wa Rais Faustin-Archange Touadéra (picha) wameteuliwa kwenye Wizara mbalimbali katika srikali hii mpya
Washirika wengi wa karibu wa Rais Faustin-Archange Touadéra (picha) wameteuliwa kwenye Wizara mbalimbali katika srikali hii mpya © ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wagombea wa zamani katika uchaguzi wa urais wameteuliwa kushikilia nafasi muhimu za uongozi.

Faustin-Archange Touadéra, rais mpya wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na Simplice Sarandji, Waziri Mkuu, "wamefaulu kwa kuteua serikali yenye baraka za raia na serikali ya watu wenye umahiri," amesema mgombea urais wa zamani.

Washirika wengi wa karibu wa raiswameteuliwa kwenye wizara mbalimbali. Naibu mkurugenzi wa kampeni za urais, Félix Moloua, ameteuliwa kuwa Waziri wa Uchumi. Charles Lemasset, msemaji wake wa kampeni za uchaguzi, ameteuliwa kuwa Waziri wa Mawasiliano. Jean Serge Bokassa, mshirika wa karibu wa Faustin-Archange Touadéra, amepwa funguo za Wizara ya Usalama wa Umma. Joseph Yakete na Charles Armel Doubane, wagombea urais wa zamani, wameteuliwa kuwa mawaziri. Yakete anashikilia Wizara ya Ulinzi wa Taifa na Doubane ameteuliwa kluwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Lakini mbali na uteuzi huu wa shukrani, hakuna mtu ambaye anakanusha kuwa watu hawa ni mahiri katika nafasi zao walizowekwa. Swali ambalo watu wengi wanajiuliza: Ni nani kati ya Waziri wa Ulinzi wa Taifa au Waziri wa Usalama wa Umma atatekeleza mchakato wa kupokonya silaha raia na kuwarejesha wapiganaji wa zamani katika maisha ya kiraia (DDR)?

Itafahamika tu kwamba baadhi ya Mawaziri walioteuliwa walihudumu kwa njia moja ima nyingine katika utawala wa François Bozizé, jambo ambalo linawatia wasiwasi baadhi ya waangalizi.

■ Orodha ya Mawaziri

Waziri wa Uchumi wa Mipango na Ushirikiano : Felix Moloua

Waziri wa Ulinzi: Joseph Yakete

Waziri wa Fedha na Bajeti: Marie Henri Dondra

Waziri wa Mambo ya Ndani, Usalama wa Umma na Utawala : Jean Serge Bokassa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda: Charles Armel Doubane

Waziri wa Sheria, Haki za Binadamu : Flavien Mbata

Waziri wa Madini na Nishati : Leopold Mboli-Fatrane

Waziri wa Mazingira, maendeleo endelevu, Maji, Misitu, Uwindaji na Uvuvi : Arlette Sombo-Dibele

Waziri wa Elimu ya Taifa, Elimu ya Juu na Utafiti : Moukadas Noure

Waziri wa Afya Afya ya Umma, na Raia : Fernande Ndjengbot

Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini : Honore Feïzouré

Waziri wa Mifugo na Afya ya Wanyama : Yerima Youssoufa Mandjo

Waziri wa Utumishi wa Umma, ufanisi wa Utawala, Kazi, Ajira na Hifadhi ya Jamii : Abdoulaye Moussa

Waziri wa Miundombinu, Usafiri, Usafiri wa Anga na Maendeleo : Theodore Jousso

Waziri wa Maendeleo ya Vijana, Maendeleo ya Michezo na mMafunzo ya Kulipenda Taifa : Silvère Ngarso

Waziri wa Posta na Mawasiliano ya kukuza Teknolojia mpya za Habari na Mawasiliano : Justin Qurna-Zacko

Waziri wa Mambo ya Jamii na Maridhiano ya Taifa : Virginia Baikoua

Waziri wa Nyumba na Maendeleo Mijini : Gaby Francky Leffa

Waziri wa Sanaa, Utalii, Utamaduni na Francophonie : Gisele Pana

Waziri wa Viwanda na Biashara: Haya Hassane

Waziri wa Mawasiliano na Habari : Charles Paul Lemasset Mandya

Waziri wa Uongozi wa Kitaifa, Sanaa na Maendeleo ya Mashirika madodgo madogo : Bertrand Touaboy

Waziri, Katibu Mkuu Kiongozi wa serikali, anayehusika na mahusiano na taasisi za Jamhuri na ufuatiliaji na tathmini ya sera za umma : Jean-Christophe Nguinza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.