Pata taarifa kuu
BENIN-UCHAGUZI-SIASA

Patrice Talon atangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais Benin

Tume huru ya Uchaguzi nchini Benin imemtangaza Patrice Talon mshindi duru ya pili ya uchaguzi wa urais uliofanyika Jumapili hii, kwa 65.39 % ya kura.

Patrice Talon (katikati ya picha akiva shati nyeupe) mjini Cotonou, Machi 20, 2016.
Patrice Talon (katikati ya picha akiva shati nyeupe) mjini Cotonou, Machi 20, 2016. © REUTERS/Charles Placide Tossou
Matangazo ya kibiashara

Patrice Talon alikua akishindana na Lionel Zinsou, Waziri Mkuu anaye maliza muda wake , ambaye amepata 34.61% ya kura. Kiwango cha ushiriki kimefikia 65.57%.

Patrice Talon, mfanyabiashara mashuhuri nchni Benini aliungwa mkono na wagombe 21 kati ya thelathini walioshindwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi.

Kabla ya matokeo hayo kutangazwa Waziri Mkuu anayemaliza muda wake, Lionel Zinsou, alikubali kuwa ameshindwa na kumpongeza mfanyabiashara Patrice Talon kwa ushindi wake.

"Matokeo ya awali yanaonyesha ushindi wa wazi wa Patrice Talon," Lionel Sinzou aliema kwa njia ya simu usiku akiliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP, akiongeza kuwa "kiwango cha ushindani ni kikubwa."

"Nimemuita Patrice Talon usiku wa kuamkia leo ili kumpongeza kwa ushindi wake, na kumtaika mafanikio mazuri na kumniweka karibu yake kwa ajili ya maandalizi ya masuala ya mpito. Nilikuwa na mazungumzo mazuri pamoja naye," alisema Waziri Mkuu anayemaliza muda wake.

Patrice Talon anamrithi Thomas Boni Yayi. Madarakani tangu mwaka 2006, kwa mujibu wa Katiba inayoruhusu mihula miwili, hakuwa mgombea katika uchaguzi huu.

Uchaguzi bila ya tukio lolote

Jumapili hii, zoezi la kupiga kura lilifanyika kwa amani. Baadhi ya wapiga kura milioni 4.7 walipiga kura katika vituo vya kupigia kura 7908 nchini humo. Mratibu wa shirikisho la mashirika la kiraia pia amekaribisha zoezi hilo lilivyofanyika kwa amani. ameuzungumzia uchaguzi huo kama "siku kuu nzuri ya uchaguzi" huku akisikitishwa kutokana na majaribio ya kujaza kura zisio halali katika masanduku ya kura katika maeneo kadhaa.

Katika duru ya pili, tuliona kuwa msongamano haukua wa kusisimua kama katika duru ya kwanza lakini wale wote ambao walihamasishwa, kwa kweli waliweza kupiga kura kwa uhuru, bila shinikizo: "Hii ni bahati hapa, tunajua kama hali kama hii haitikei katika nchi nyingi za Afrika. Tunaridhika na demokrasia yetu," amesema mpiga kura mmoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.