Pata taarifa kuu
BENIN-UCHAGUZI-SIASA

Benin: duru ya pili ya uchaguzi wa urais yafanyika

Duru ya pili ya uchaguzi imefanyika Jumapili hii Machi 20 nchini Benin, ambapo wapiga kura milioni 4.7 wameshiriki katika uchaguzi huu.

Mtu hyu akitumbukiza kadi yake ya kura katika sanduku ya kupigia kura, katika kituo cha kupigia kura cha Cotonou, MAchi 20, 2016.
Mtu hyu akitumbukiza kadi yake ya kura katika sanduku ya kupigia kura, katika kituo cha kupigia kura cha Cotonou, MAchi 20, 2016. © PIUS UTOMI EKPEI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wanatakiwa kumchagua mtu mmoja kati ya Waziri Mkuu Lionel Zinsou na mfanyabiasha Patrice Talon, kwa kumrithi Thomas Boni Yayi, ambaye ametamatisha muhula wake wa pili.

Wagombea hawa wanaonekana kuwa ushindani wao ni wa kiwango kidogo, baada ya duru ya kwanza na mashaka bado yapo. Katika vituo vya kupigia kura katika miji ya Cotonou na Abomey-Calavi ambavyo vimefunguliwa mapema asubuhi, wapiga kura wanaonekana kuwa na nia ya kutaka kura zao zihesabiwe vilivyo.

Katika kituo cha kupigia kura kilichowekwa katika shule ya Fidjrosse ya Kati, eneo lenye watu wengi, karibu na uwanja wa ndege wa Cotonou, mpigaji kura wa kwanza alitumbukiza kura yake saa 7:00 asubuhi. Sawa na katika eneo jingine lenye watu wengi, nje kidogo na mji wa Cotonou.

Kila kimewekwa mahali pake. Kwenye kadi moja ya kura, picha na nembo ya wagombea hao wawili vimewekwa. Wawakilishi wa wagombea wote hao walikuwepo, pamoja na wale wa Mahakama ya Katiba.

Katika duru ya kwanza, kutokana na utata juu ya usambazaji wa kadi za wapiga kura, raia wengi wa Benin walikuwa na wasiwasi mapema Jumapili mchana. Kisha wasiwasi huo uliondoka hatua kwa hatua. Leo mtu anahisi kwamba hakuna wasiwasi hasa lakini kulikuepo na utulivu mkubwa miongoni mwa wapiga kura. Wapiga kura wamekua ni "wenye kusubiri kwa kufanya wajibu wao wa kiraia," kama wanavyopenda kusema. Kila mtu ameonyesha uamuzi wake au msimamo wake, wanaonekana kuwa na imani kati yao, kuhamasishwa, kuwa na msimamo na kuwa umakini.

Uchaguzi Abomey-Calavi

Calavi ni wilaya yenye watu wengi nchini kote Benin na iko katika idara yenye wapiga kura wengi, zaidi ya 700 000. Katika ukumbi wa mji wa Calavi, vituo vya kupigia kura kumi na moja vimefunguliwa saa 7.

Uwezekano wa udanganyifu

Kama kwa katika duru ya kwanza, wapiga kura waliweza kupiga kura ama kwa kitumia kadi ya zamani ya mpiga kura, ile ya mwaka 2015, au kwa kutumia kadi mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.