Pata taarifa kuu
WHO-ZIKA-AMERIKA

Kuenea kwa virusi vya Zika, WHO yatangaza hali ya dharura kidunia

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa madhara makubwa wanayopata watoto wanaozaliwa kusini mwa nchi za Amerika kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na virusi vya Zika, na kwamba ugonjwa huwa sasa unatangazwa kama hali ya dharura kimataifa.

Mkurugenzi wa shirika la afya duniani, WHO, Margaret Chan, akizungumza hapo jana mjini Geneva
Mkurugenzi wa shirika la afya duniani, WHO, Margaret Chan, akizungumza hapo jana mjini Geneva
Matangazo ya kibiashara

WHO inasema kuwa kesi zinaotokana na vizuri hivyo na kusababisha athari kubwa kwa watoto wanaozaliwa ikiwa ni pamoja na kuwa na vichwa na ubongo mdogo, ni wazi kwa sehemu unasababishwa na mbu wanaobeba virusi vya Zika, hivyo linalazimika kutangaza hali ya dharura kidunia.

WHO imejikuta kwenye shinikizo kubwa la kuchukua hatua za haraka kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huu baada ya kukiri kuwa haikuchukua hatua madhubuti wakati ugonjwa wa virusi vya Ebola ulipozuka kwenye nchi za Afrika Magharibi.

Mkuu wa shirika hilo, Margareth Chan, amesema kuwa mkutano wa wataalamu ambao huketi kama kamati ya dharura, wamekubaliana kwa kauli moja kuwa, kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya maambukizi ya Zika wakati wa ujauzito na kwamba microcephaly ni chanzo kikuu licha ya kuwa hakuna uthibitisho wa kisayansi uliofanywa.

Virusi vya Zika
Virusi vya Zika REUTERS/Josue Decavele

WHO juma moja lililopita ilionya kuwa vizuri vinavyotokana na mbu, vimeanza kuenea kwa kazi kwenye bara la Amerika, na kwamba huenda nchi za ukanda zikapokea wagonjwa zaidi ya milioni nne mwaka huu.

Ni miongo kadhaa sasa imepita toka ugonjwa wa Zika ulipogunduliwa kwa mara ya kwanza nchini Uganda mwaka 1947 nwa kwamba virusi hivi havikuwa tishio sana nwa kwamba vilikuwa vinasababisha homa kali.

Licha ya dalili zake mpaka sasa kutowekwa wazi moja kwa moja, lakini kuongezeka kwa matatizo ya mishipa ya fahamu kunafanya shirika hilo kuguswa na hali ilivyo na hivyo kutangaza hali ya dharura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.