Pata taarifa kuu
ULAYA-AFRIKA-WAHAMIAJI-USALAMA

Mkutano juu ya Uhamiaji Malta: makubaliano juu ya umuhimu wa kuchukua hatua

Siku ya kwanza ya mkutano juu ya uhamiaji nchini Malta imemalizika Jumatano kwa viongozi wa Ulaya na Afrika kuchangia chakula cha jioni.

Picha za viongozi wa Ulaya na wenzao wa Afrika kuhusu maendeleoya Ulaya na Afrika kwa kuzuia suala la uhamiaji, Valletta, Novemba 11, 2015.
Picha za viongozi wa Ulaya na wenzao wa Afrika kuhusu maendeleoya Ulaya na Afrika kwa kuzuia suala la uhamiaji, Valletta, Novemba 11, 2015. REUTERS/Darrin Zammit Lupi
Matangazo ya kibiashara

Mkutano unaendelea leo Alhamisi ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa mfuko pamoja wa euro bilioni 1.8 kufadhili miradi ya maendeleo na usimamizi wa uhamiaji katika bara la Afrika.

Ufunguzi uligubikwa na makubaliano juu ya haja ya kuacha kuzuia vifo katika bahari au katika jangwa, njia wanazotumia wahamiaji au wakimbizi.

Usiku wa Jumatano wiki hii zaidi ya viongozi sitini kutoka Afrika na Ulaya, walisalia kimya kwa dakika moja kwa kutoa heshima zao kwa wahamiaji na wakimbizi waliokufa maji kufuatia kuzama kwa meli ziliokua zikiwasafirisha katika bahari ya Mediterranean. Katika dakika moja hiyo ya kusalia kimya iliyotekelezwa na marais na viongozi hao wa serikali kabla ya mazungumzo, siku hiyo ya kwanza ya mkutano wa kilele nchini Malta ilikua kwanza siku ya makubaliano.

Makubaliano juu ya kuzuia vifo, na maeneo wanayotumia kwa kuingia Ulaya. Makubaliano,pia, kuhusu suala la kuboresha hali ya maisha barani Afrika, ikiwa ya kisiasa au kiuchumi, inaweza kuchangia kukomesha wimbi la wakimbizi au wahamiaji kuingia Ulaya.

Kwa uwezo wa kutekeleza upande mwingine, misimamo ilitofautiana. Tangu kuanza kwa mazungumzo, upande wa Ulaya, wamekua wakitoa wito kwa nchi wanakotokea wakimbizi na wahamiaji kuzingatia kuendeleza uchumi wao na kuboresha utawala bora, hasa katika suala la vyomvo vya sheria na kuheshimu haki za binadamu.

Waafrika wapiga kidole kwenye meza

Upande wa Afrika, hata hivyo, kupitia rais wa Tume ya Afrika, wametaka kuweka suala la uhamiaji wa Afrika katika mazingira ya historia ndefu ya mahusiano kati ya mabara mawili.

"Afrika pia iliwapokea wahamiaji na wakimbizi wa Ulaya, hata kabla ya ukoloni, amesema Nkosazana Dlamini-Zuma. Wakati na baada ya Vita vikuu vya II, wakimbizi wa Ulaya, wale waliotafuta hifadhi na na raia wengine wa Ulaya walikimbilia hadi kwenye eneo la kusini la Afrika kwa sababu za kibiashara au kwa kuishi. Walipokelewa. Wakati huo, hakukuwa na mgogoro wa wahamiaji wa Ulaya barani Afrika", amesema Nkosazana Dlamini-Zuma.

Rais wa Senegal Macky Sall, kwa niaba ya ECOWAS na Rais wa Niger Mahamadou Issoufou, pia waliweka wazi kwamba busara ni jambo moja, lakini fedha ili kukidhi mahitaji ya Ulaya ni jambo jingine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.