Pata taarifa kuu
GHISLAINE-CLAUDE-MAUAJI-USALAMA

Ghislaine Dupont na Claude Verlon, miaka miwili baada ya kuuawa

Novemba 2, 2013, waandishi wa habari wa RFI waliotumwa kaskazini mwa Mali, Ghislaine Dupont na Claude Verlon walitekwa nyara na kuuawa karibu na mji wa Kidal.

Picha za Claude Verlon na Ghislaine Dupont.
Picha za Claude Verlon na Ghislaine Dupont. RFI
Matangazo ya kibiashara

Miaka miwili baada ya mauaji hayo, hakuna uchunguzi ambao umekwishafanyika wakati ambapo ulimwengu unasherehekea Siku ya Kimataifa ya kukomesha visa vya kutoadhibu uhalifu dhidi ya waandishi wa habari.

Miaka miwili iliyopita, Jumamosi, Novemba 2, 2013, Ghislaine Dupont na Claude Verlon waliuawa katika wakitokea Kidal kaskazini mwa Mali, wakati ambapo walikuwa wakiandaa mfululizo wa ripoti kuhusu uchaguzi wa wabunge nchini Mali, mauaji ambayo siku chache baadaye yalidaiwa kutekelezwa kundi la wanamgambo wa kiislamu la Aqmi. Siku hii ni ya huzuni kwa wale wote ambao waliwafahamu waandishi hao wa habari na tarehe hii pia inaashira Siku ya Kimataifa ya kukomesha visa vya kutoadhibu uhalifu dhidi ya waandishi wa habari na hivyo, Umoja wa Mataifa uliamuru kupitia azimio liliyopitishwa Desemba 18, 2013, kutoa heshima kwa wanahabari wenzetu.

Kama linavyokumbuka Shirika la waandishi wa habari Wasiokuwa na Mipaka (RSF), waandishi wa habari mia saba na kumi na nane waliuawa katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, mia na thelathini na nne tangu mauaji ya Ghislaine na Claude, uhalifu ambao, umejaa dhuluma, umesalia bila kuadhibibwa katika matukio mengi. " Kupiga vita dhidi ya visa vya kutoadhibu ni muhimu kwa sababu zaidi ya 90% ya uhalifu uliofanywa dhidi ya waandishi wa habari duniani haujaadhibiwa ", amesema Christophe Deloire, katibu mkuu wa RSF. Anaamini pia kwamba ukatili ni " kama motisha kwa wale wanaotekeleza vitendo hivi."

Uchunguzi unafanywa kwa mwendo wa kinyonga

Kwa sasa, mauaji ya Ghislaine Dupont na Claude Verlon yamewekwa katikambaya katika jamii moja uhalifu ambao haujaadhibiwa. Miezi kumi na nane baada ya kuanzishwa uchunguzi wa mahakama, wauaji bado hawajajulikana, wala wale ambao waliamuru mauaji hayo, wala kutojua ni katika mazingira gani wenzetu waliuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.