Pata taarifa kuu
TANZANIA-UCHAGUZI-SIASA

Tume ya Uchaguzi kuanza kutoa matokeo ya kwanza Jumatatu

Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania imesema itaanza kutoa matokeo rasmi ya uchaguzi wa urais leo Jumatatu saa tatu saa za Afrika mashariki katika jumba la mikutano la Julius Nyerere, Dar es Salaam. Hata hivyo kuna maeneo ambayo uchaguzi haukufanyika Jumapili Oktoba 25.

Zoezi la uhesabuji wa kura limeanza shughuli katika kituo kimojacha kupigia kura Dar es Salaam, Oktoba 25, 2015.
Zoezi la uhesabuji wa kura limeanza shughuli katika kituo kimojacha kupigia kura Dar es Salaam, Oktoba 25, 2015. AFP/DANIEL HAYDUK
Matangazo ya kibiashara

Kituo cha Kimara Stop Over jijini Dar es Salaam ambako uchaguzi utarejelewa kufanyika leo Jumatatu baada ya kutatizika Jumapili Oktoba 25.Katika eneo hilo wapiga kura waliyachoma makaratasi ya kupigia kura . Hadi saa 12 asubuhi leo Jumatatu maafisa wa kusimamia uchaguzi walikua bado hawajafika kituoni.

Mjini Mwanza, kaskazini magharibi mwa Tanzania, masanduku ya kura yanaendelea kukusanywa katika afisi kuu kabla ya kuanza kwa shughuli ya kuhesabu kura.

Itafahamika kwamba katika uchaguzi huo wa Jumapili Oktoba 25, watu walijitokeza kwa wingi katika uchaguzi unaotajwa kuwa na ushindani mkubwa huku muungano mpya wa upinzani ukijaribu kukiondoa madarakani chama tawala CCM kilichoshikilia madaraka kwa miaka 54.

Katika maeneo mengine ,upigaji kura uliongezewa muda ili kuwapa fursa wapiga kura walio katika milolongo mirefu kupiga kura.

Polisi wamewasifu watu kwa kupiga kura kwa salama, maneno ambayo pia yalikaririwa na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, Ramadan Kailima hapo awali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.