Pata taarifa kuu
TANZANIA-UCHAGUZI-SIASA

Tanzania: Mahakama kuu kutoa uamzi kuhusu kifungu tata

Mahakama kuu nchini Tanzania leo Ijumaa inatazamia kutoa maamuzi kuhusu tafsiri ya kifungu tata cha sheria ya uchaguzi ikiwa mpiga kura asalie mita 200 baada ya kupiga kura au aende nyumbani.

Moja ya mita ya Dar es Salaam, mji mkuu wa Tanzania ambako kunasubiriwa uamzi wa Mahakama kuu kuhusu kifungo tata.
Moja ya mita ya Dar es Salaam, mji mkuu wa Tanzania ambako kunasubiriwa uamzi wa Mahakama kuu kuhusu kifungo tata. Bruno Minas / RFI
Matangazo ya kibiashara

Upinzani ulikwenda Mahakamani kutaka sheria hiyo kutafsiriwa ikiwa na lengo la kuwaruhusu wapiga kura kusalia mita 200, kwa kile Unachosema ni kulinda kura.
Hata hivyo, serikali na tume ya uchaguzi kupitia mawakili wake wanasema wapiga kura waende nyumbani baada ya kupiga kura.

Wakati huo huo wito umeendelea kutolewa kwa raia wa nchi hiyo kujitokeza kwa wingi kutekeleza jukumu lao la kidemokraia.
Wapiga kura Milioni 22 wanatarajiwa kupiga kura katika uchaguzi huu unaonekana kuwa utakuwa na ushindani mkali kati ya mgombea wa CCM John Pombe Magufuli na mgombea wa upinzani Edward Lowasa.

Martina Kabisama Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Mashirika ya haki za binadamu Kusini mwa Afrika SAHRINGON, amewaambia Watanzania kutekeleza haki yao ya kimsingi kwa kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili na kupiga kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.