Pata taarifa kuu
TANZANIA-UCHAGUZI-SIASA

Tanzania: kampeni za uchaguzi zafikia ukingoni wiki hii

Kampeni kuelekea uchaguzi Mkuu nchini Tanzania siku ya Jumapili juma hili zimeingia katika kipindi cha lala salama.

Moja ya mitaa ya Dar es Salaam.
Moja ya mitaa ya Dar es Salaam. Bruno Minas / RFI
Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa juma lililopita kulikuwa na mdahalo wa wagombea urais jijini Dar es salaam kati ya wagombea 8 wanaowania urais nchini humo, mgombea wa chama tawala CCM na CHADEMA hawakuhudhuria.

Wagombea wote wanaahidi mabadiliko ikiwa watashinda uchaguzi huo na kinyanganyiro kinatarajiwa kuwa kati ya mgombea wa chama tawala John Pombe Magufuli na mgombea wa upinzani, CHADEMA Edward Lowasa.

Watanzania wamekuwa wakihimizwa kudumisha amani kipindi hiki cha uchaguzi.

Hayo yakijiri Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Tanzania,hivi karibuni ilimwandikia barua ya kumwonya mgombea mweza wa chama cha upinzani CHADEMA, Juma Duni Haji, kwa kile inachosema imevunja maadili ya uchaguzi. Tume hiyo inasema mgombea huyo mwenza amepotosha umma kwa kudai kuwa tume imeongeza vituo hewa zaidi ya elfu 20 vya kupigia kura.

Mwenyekiti wa Kamati ya maadili katika tume hiyo Jaji Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid aliiambia Idhaa ya Kiswahili ya RFI kwamba siku ya Jumamosi walikuwa na kikao na vyama vyote kuhusu suala la maadili lakini Chama cha CHADEMA hakikutuma mwakilishi.

Kampeni za uchaguzi nchini Tanzania zimeingia katika kipindi cha lala salama na raia wa nchi hiyo wanatarajiwa kupiga kura Jumapili ijayo, na katika barabata za jijini la Dar es salaam bendera za chama tawala CCM na kile cha upinzani CHADEMA zinaonekana kila kona. Zaidi ya wapiga kura Milioni 22 watashiriki katika zoezi hilo la kihistoria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.