Pata taarifa kuu
UN-USHIRI-USALAMA

UN mbioni kupata askari 40,000 wa ziada

Zaidi ya nchi hamsini zimeahidi Jumatatu wiki hii kutoa askari 40,000 wa ziada kwa Umoja wa Mataifa.Chini ya ushawishi wa Marekani, zaidi ya nchi hamsini zimeahidi Jumatatu wiki hii kutoa askari 40,000 wa ziada, wakati ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani unaendelea kukabiliwa na visa mbalimbali pamoja na mazingira magumu.

Askari wa kulinda amani nchini Mali (Minusma), hapa ni katika mji waKidal, 22 Julai mwaka 2015.
Askari wa kulinda amani nchini Mali (Minusma), hapa ni katika mji waKidal, 22 Julai mwaka 2015. REUTERS/Adama Diarra
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani Barack Obama aliitisha pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York mkutano kuhusu njia za kuimarisha tume 16 za Umoja wa Mataifa duniani kote, ambapo tayari 125,000 askari wa umoja wa Mataifa wamepelekwa katika nchini mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wanajeshi, askari polisi na raia wa kawaida kutoka nchi 124.

Mtandao huu, amesema Obama "hautoshi kwa mahitaji ambayo yanaongezeka siku baada ya siku" kutokana na kuenea kwa migogoro barani Afrika (Mali, Sudan Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo). Askari wa kulinda amani pia wanakabiliwa na mashambulizi mbalimbali: siku moja kabla ya mkutano huo, askari wa kulinda amani kutoka Afrika Kusini aliuawa katika jimbo la Darfur, nchini Sudan Kusini.

Askari wa Minusma wakipiga doria katika mji wa Kidal, Julai 23, 2015.
Askari wa Minusma wakipiga doria katika mji wa Kidal, Julai 23, 2015. REUTERS/Adama Diarra

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma) unakabiliwa na mashambulizi mbalimbali katika historia ya Umoja wa Mataifa, pamoja na vifo 60 tangu kupelekwa kwake nchini humo.

" Kuimarisha na kuleta mageuzi katika kulinda amani "

" Tupo hapa leo ili kuimarisha na kulta mageuzi katikakulinda amani kwani usalama wetu wa pamoja unategemea ", amesema Barack Obama. Marekani ni mfadhili mkubwa katika kulinda amani, ambapo imekua ikitoa asilimia 28% katika bajeti ya kila mwaka ya dola bilioni 8.3, lakini imekua ikisita kuchangia kwa askari. Barack Obama ametangaza mara dufu ya idadi ya maafisa wa Marekani (kwa sasa 78) ambao wanahudumu chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa. "Mataifa zaidi yanapaswa kuchangia na kutoa majeshi zaidi," amesisitiza.

China imesema iko tayari kutoa askari polisi 8000 na Colombia askari 5000, ambapo hadi sasa imekua bado haijachangia katika sekta hii. Uingereza itamtuma zaidi ya askari mia moja nchini Somalia na Sudan kusini. Uholanzi imeongeza muda wa kushiriki katika kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma) kwa mwaka mmoja na imeahidi kuongeza ufadhili wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.