Pata taarifa kuu
BUKINA FASO-MAPINDUZI-USALAMA-SIASA

Burkina Faso: mshirika wa karibu wa Compaoré akabidhiwa mamlaka

Wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Rais (RSP) wametangaza Alhamisi wiki hii kwamba wamewanga'tua mamlakani viongozi wa mpito nchini Burkina Faso. Wamehakikisha kuwa waanataka kuandaa "Uchaguzi wa umoja."

Jenerali Gilbert Diendéré hapa mwaka 2011, mmoja wa wanajeshi waliongoza mapinduziya kijeshi nchini Burkina Faso, Septemba 17, 2015.
Jenerali Gilbert Diendéré hapa mwaka 2011, mmoja wa wanajeshi waliongoza mapinduziya kijeshi nchini Burkina Faso, Septemba 17, 2015. AFP PHOTO / AHMED OUOBA
Matangazo ya kibiashara

Tangu Jumatano mchana wiki hii, kundi la wanajeshi waliofanya mapinduzi likiongozwa na jenerali Gilbert Diendéré, mshirika wa karibu wa Rais wa zamani wa Burkina Faso, Blaise Compaoré, wameendelea kuwashikilia viongozi wa serikali, ikiwa ni pamoja na Rais Michel Kafando na Waziri Mkuu Isaac Zida.

Wakati huo huo jenerali Gilbert Diendéré ametangazwa kuwa kiongozi mpya wa taifa hilo na walinzi wa rais waliofanya mapinduzi ya kijeshi.

Taarifa iliyotolewa na walinzi hao imesema Jenerali Gilbert Diendere, aliyekuwa mkuu wa majeshi katika utawala wa Blaise Compaoré, ndiye atakayekuwa rais mpya.

Tangazo la awali kupitia runinga ya taifa lilisema mashauriano yangefanyika kuunda serikali mpya ya mpito ambayo ingeandaa “uchaguzi wa amani na wa kuhusisha wote”.

Spika wa bunge la mpito Cheriff Sy amesema kilichofanyika ni “mapinduzi ya serikali”.

Hata hivyo ufyatulianaji wa risasi umeanza kushuhudiwa katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.

Rais Francois Hollande ameshutumu hatua ya walinzi hao wa rais ya kupindua serikali.

Walinzi hao wanadaiwa kuwafyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wakiandamana Ouagadougou wakipinga hatua ya wanajeshi hao ya kufanya mapinduzi ya kijeshi, huku baadhi wakikamatwa.

Wanajesi hao wametangaza amri ya kutotoka nje usiku nchini humo, na kufunga mipaka ya taifa hilo, shirika la habari la Ufaransa la AFP limeripoti.

Makao makuu ya chama cha Blaise Compaoré cha Congress for Democracy and Progress (CDP) yalivamiwa na waandamanaji na kuporwa, baada ya habari za mapinduzi hayo kuenea.

Rais Hollande amewataka wanajeshi waliofanya mapinduzi hayo kumuachilia mara moja Rais wa mpito Michel Kafando na Waziri Mkuu Isaac Zida, waliozuiliwa wakiongoza mkutano wa baraza la mawaziri katika Ikulu ya rais Jumatano wiki hii.

Serikali yao ya mpito ilitarajiwa kukabidhi mamlaka kwa serikali ambayo ingechaguliwa kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 11.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.