Pata taarifa kuu
CAF-SOKA-AFRIKA

Senegal yaongoza katika kundi K

Jumamosi Septemba 5, kumeshihudiwa mechi mbalimbali katika viwanja tofauti vya soka barani Afrika. Michuano hii ya makundi kufuzu katika fainali za mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon imeingia Jumamosi hii katika siku yake ya pili.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Senegal, Lamine Gassama na Kara Mbodji.
Wachezaji wa timu ya taifa ya Senegal, Lamine Gassama na Kara Mbodji. AFP PHOTO / CARL DE SOUZA
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuishinda Burundi kwa mabao (3-1) katika mchezo wa siku ya kwanza, Senegal inaendelea kufanya vizuri katika michuano ya kufuzu Kombe la mataifa ya Afrika. Simba, wameshambulia mara kadhaa na kutawala mpira dhidi ya Namibia, hadi kipenga cha mwisho, Namibia walijikua wakiangukia pua kwa kufungwa mabao 2 kwa 0, na kupelekea Senegal kuendelea kufanya vizuri katika michuano hii.

Bao la kwanza la Senegal limefungwa na Cheikhou Kouyaté katika dakika ya 36 ya mchezo, huku bao la pili likiwekwa kimyani na Sadio Mané katika dakika 56.

Kwa sasa Senegal inaongoza katika kundi K kwa alama 6.

Kwa upande mwengine Burundi ikiwa nyumbani, imeiadhibu Niger kwa kuifunga mabo 2 kwa 0. Kwa sasa Burundi inachukua nafasi ya pili katika kundi K, ikiwa na alama tatu, baada ya Senegal.

Djibouti imeangukia pua kwa kufungwa na Togo mabao 2 kwa 0, huku Uganda ikiiadhibu Comoros kwa bao 1 kwa 0.

Rwanda ikiwa katika uwanja wake wa Amahoro imeangukia pua kwa kufungwa na Ghana kwa bao 1 Kwa 0, huku Tanzania ikiwa nyumbani ikalazimika kwenda sare ya kutofungana na Nigeria.

Seychelles imekwenda sare ya kufungana bao 1 kwa 1 na Ethiopia, huku Tunisia ikikubali kichapo cha bao 1 kwa 0 dhidi ya Liberia.

Botswana imeiadhibu Burkina Faso kwa bao 1 kwa 0, huku Congo - Brazzaville ikiimenya Guinea Bissau kwa mabao 4 kwa 2 katika siku ya pili ya michuano ya kufuzu Kombe la mataifa Afrika.

Wakati huo huo Morocco imefanikiwa kuiadhibu Sao Tome Principe kwa mabao 3 kwa 0.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.