Pata taarifa kuu
UN-CAR-SANGARIS-UHALIFU-HAKI

Tume ya haki za binadamu ya UN yalaumu baadhi ya askari wa UN

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, ameeleza kuchukuziwa na ripoti za hivi karibuni zikiwatuhumu wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa kutekeleza vitendo vya udhalilishaji na ubakaji dhidi ya wasichana na watoto.

Askari kumi na nne wa Ufaransa walioko kwenye operesheni Sangariswanatuhumiwa katika kesi za unyanyasaji wa kijinsia, lakini wachache wametambuliwa.
Askari kumi na nne wa Ufaransa walioko kwenye operesheni Sangariswanatuhumiwa katika kesi za unyanyasaji wa kijinsia, lakini wachache wametambuliwa. AFP PHOTO / MARCO LONGARI
Matangazo ya kibiashara

Akiwa katika ziara ya kikazi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, mkuu wa tume hiyo, Zeid Ra'ad Al-Hussein ambaye amesema ameshtushwa na ripoti hizi ambazo anasema zinatia hofu kuhusu mwenendo wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa.

Ra'ad Al-Hussein amesema tuhuma dhidi ya wanajeshi wa Ufaransa walioko kwenye operesheni Sangaris pamoja na tuhuma za hivi karibuni dhidi ya msichana mmoja ambaye inadaiwa tayari amejifungua, zinasikitisha ambapo ameongeza kuwa hatua lazima zichukuliwe mapema dhidi ya waliohusika.

Wakati huohuo kesi mpya ya madai ya ubakaji kwa askari wa Ufaransa wa kikosi kinachoendesha operesheni Sangaris nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imewekwa wazi.

Pia kwa mujibu wa Ra'ad Zeid Al-Hussein, viongozi wa Ufaransa walipewa taarifa ya kesi hii. Madai haya ni pamoja na mfululizo wa mashtaka ya ubakaji unaofanywa na askari wa kigeninchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. vyombo vya sheria vya Ufaransa vilianzisha uchunguzi kuhusu madai hayo ya ubakaji yaliofanywa na askari 14 wa Ufaransa katika mji wa Bangui mwaka 2014. Askari wengine watatu kutoka barani Afrika pia walihusishwa na ripoti ya Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.