Pata taarifa kuu
KA KUSINI-MALEMA-SHERIA

Afrika Kusini: kesi ya kashfa ya rushwa dhidi ya Malema yafutwa

Kiongozi wa chama cha "wanaharakati wanaotetea uhuru wa uchumi" (EFF), Julius Malema, hafuatiliwi tena na vyombo vya sheria vya Afrika Kusini kwa tuhuma za kashfa za rushwa kwa sababu ya kuahirishwa mara kadhaa kwa kesi yake iliyoanza miaka mitatu iliyopita.

Baada kesi yake kuahirishwa mara kadhaa, Jaji ameamua kufuta mashtaka dhidi ya Julius Malema, hapa ni Agosti 3 katika mahakama ya Polokwane.
Baada kesi yake kuahirishwa mara kadhaa, Jaji ameamua kufuta mashtaka dhidi ya Julius Malema, hapa ni Agosti 3 katika mahakama ya Polokwane. AFP PHOTO / MUJAHID SAFODIEN
Matangazo ya kibiashara

Uamzi huo umechukuliwa Jumanne wiki hii na jaji wa Afrika Kusini Billy Mothle .

" Kwa sasa, faili hii imefungwa na uko huru tangu sasa ", amesema Jaji Billy Mothle, akimwambia Julius Malema katika mahakama ya Polokwane (kaskazini). " Tangu mwaka 2012, washitakiwa walisubiri kuhukumiwa. Ni muda mrefu sana kwa mtu yeyote na sitaki kuongeza muda ", amesema jaji Billy.

Kesi hii, tayari kuahirishwa miezi kadhaa tangu mwezi Septemba mwaka 2015, iliahirishwa tena Jumatatu, Agosti 3 kutokana na kulazwa hospitali kwa mmoja wa washitakiwa. Jumanne wiki, upande wa mashtaka uliomba vikao viweze kuanza bila kuwepo kwa mshitakiwa huyo au kesi hio iahirishwe kwa mara nyingine tena. Lakini hoja zote hizi zilikataliwa na jaji.

Kesi hii ilianza tangu mwaka 2009

Julius Malema alishtakiwa tangu miaka mitatu iliopita kwa kujitajirisha kinyume cha sheria wakati wa zabuni la wizi la Euro milioni 3,7, kwa ajili ya kukarabati barabara katika mkoa wa Limpopo, kaskazini mwa Afrika Kusini. Kesi hiyo ilianza mwaka 2009.

Kama Julius Malema yuko huru, serikali inaweza kuamua kumfuatilia upya, ili mradi ianzishe utaratibu mpya. " Kama wanataka kufungua upya utaratibu wana haki ya kufanya hivyo! Sina hofu nao ",amesema Julius Malemahuku akipongezwa na umati wa wafuasi wake waliokua nje ya mahakama ya Polokwane. " Najua kwamba watapata kitu kingine kipya kwa sababu wao ni mbwa ", ameongeza Malema akikilenga chama tawala cha ANC,wakati kesi hiyo haihusiani na chama hicho.

Itafahamika kwamba Julius Malema alifukuzwa katika chama cha ANC mwaka 2012.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.