Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-USALAMA

Burundi: Agathon Rwasa achaguliwa kuwa naibu spika wa kwanza wa Bunge

Nchini Burundi, Agathon Rwasa amechaguliwa kuwa naibu spika wa kwanza wa Bunge kwa kura 108 kwa jumla ya kura 112, ikiwa ni pamoja na kura za wabunge kutoka chama tawala cha Cndd-Fdd.

Agathon Rwasa, mmoja miongoni mwa viongozi wakuu wa upinzani.
Agathon Rwasa, mmoja miongoni mwa viongozi wakuu wa upinzani. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Agathon Rwasa alikua miongoni mwa viongozi wa upinzani ambao wamekua wakilaani muhula wa tatu wa Pierre Nkurunziza katika uchaguzi wa urais. Alikua akithibitisha kutotambua matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika Julai 21 mwaka 2015.

Mwezi Septemba mwaka 2006, rais Pierre Nkurunziza (kulia) na kiongozi wa FNL Agathon Rwasa, walitia saini kwenye Mkataba wa amani jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mwezi Septemba mwaka 2006, rais Pierre Nkurunziza (kulia) na kiongozi wa FNL Agathon Rwasa, walitia saini kwenye Mkataba wa amani jijini Dar es Salaam, Tanzania. (Photo: AFP)

Mchakato huo wa kuwachagua viongozi wa Bunge uliendeshwa kwa kasi katika siku za hivi karibuni nchini Burundi. Mpinzani mkuu wa Burundi, Agathon Rwasa, alishiriki katika kikao cha kwanza cha Bunge siku ya Jumatatu wiki hii. Leo Alhamisi uchaguzi wa viongozi wa Bunge umefanyika kwa haraka. Katika Bunge hili ambalo linatawaliwa na chama tawala ambacho chenye wabunge 86 kwa jumla ya wabunge 121, huku Agathon Rwasa akiwa na wabunge wasizidi 19. Lakini hakukuwepo na mjadala. Uchaguzi umefanyika kwa haraka na Agathon Rwasa, ambaye alikuwa tu mgombea wa nafasi ya naibu wa kwanza wa spika wa Bunge, amechaguliwa kwenye nafasi hiyo.

Hii ni ishara ya makubaliano kati ya serikali na Agathon Rwasa. Kulikuwa na mgombea mmoja tu kwa kila nafasi. Nyabenda Pascal, kiongozi wa cha Cndd-Fdd alikuwa mgombea pekee kwa nafasi ya spika wa Bunge na waziri wa mambo ya ndani Edouard Nduwimana alikua mgombea pekee wa nafasi naibu wa pili wa spika wa Bunge. Jambo hili imeonekana kama ni ishara ya kuupa nafasi upinzani. Ishara nyingine ya makubaliano hayo, Agathon Rwasa amechaguliwa kwa kura nyingi kuliko kiongozi wa chama cha Cndd-Fdd, Pascal Nyabenda. Agathon Rwasa alipata kura 108, wakati Pascal Nyabenda akipata 101.

Watu wengi wamekua wakijiuliza Agathon Rwasa atapata nini baada ya kukubali kushirikiana na Cndd-Fdd?? Mpaka sasa hakuna anayejua. Hata hivyo, alipoingia katika taasisi hiyo watu wengi walipigwa na mshangao mkubwa nchini Burundi na chama chake kimegawanyika kati ya wafuasi wanaopongeza uamzi wake na wale wanaoulaani. Hili ni pigo kubwa kwa upinzani kwa kujihisi yatima baada ya kumpoteza mmoja kati ya wapinzani wake wakuu. Hata hivyo, chama cha Uprona, kisiotambuliwa na serikali ambacho kiliongana na Agathon Rwasa hakijajua karata gani kitacheza wakati ambapo serikali imekua ikishangilia, ikibaini kwamba kukubali kwa Agathon Rwasa kuingia Bungeni ni ushindi mkubwa kwa upande wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.