Pata taarifa kuu
UNESCO-ISIL

UNESCO yalaani uharibufu wa maeneo ya asili unaofanywa na wapiganaji wa ISIL nchini Syria, Iraq na Mali

Shirika la Umoja wa mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, juma hili limetoa kauli kulaani vitendo vinavyofanywa na kundi la kiislamu la ISIL ambalo wapiganaji wake wameendelea kuharibu maeneo ya utamaduni na urithi wa dunia.

Moja ya eneo la urithi wa dunia lililoko mjini Palmyre, Syrie
Moja ya eneo la urithi wa dunia lililoko mjini Palmyre, Syrie Unesco/G. Degeorges
Matangazo ya kibiashara

UNESCO inasema kuwa vitendo vinavyofanywa na kundi la ISIL havikubaliki na kwamba vitendo hivyo vinaweza kuhesabiwa kama makosa ya uhalifu wa kivita.

Wakiendelea na mkutano wao mjini Bonn, Ujerumani, wakuu wa shirika hilo na nchi nyingine wanachama wamelaani vikali matukio ya uharibufu unaofanywa na kundi hilo kwenye maeneo ya kihistoria nchini Iraq, Syria, Afghanistan na Mali.

Shirika hilo linasema kuwa mashambulizi ya kimataifa dhidi ya majengo ya kidini, shule, utamaduni, sayansi na yale ya kusaidia raia pamoja na majengo ya kihistoria, ni matukio ambayo yanaweza kutafsiriwa kama uhalifu wa kivita.

Mwezi April mwaka huu, kundi la ISIL lilitoa mkanda wa video ikionesha wapiganaji wake wakitumia risasi na mapanga kuharibu vitu vya kihistoria mjini Harta, huku picha nyingine zikiwaonesha wakiharibu majengo ya kihistoria nchini Iraq kwenye mji wa Nimrud na msikiti wa Mosul.

UNESCO pia imeonesha wasiwasi wake kwa kundi hilo kuwa huenda likaharibu mji wa kihistoria na hifadhi ya dunia wa Palmyra nchini Syria, mji ambao waliuteka mwezi May mwaka huu.

Shirika hilo limeongeza kuwa maeneo mengine ya urithi wa dunia nchini Afghanistan, Ira, Libya, Mali, Syria na Yemen nayo yako hatarini kuharibiwa kutokana na harakati zianzoendelea kufanywa na kundi la ISIL.

Wakuu wa UNESCO wanakutana kwenye mkutano wao wa 39 wa kamati kuu ambapo watajadili na kupitia mao,bi mapya 36 ya asili na utamaduni ambayo yanataka yaainishwe kama maeneo ya urithi wa dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.