Pata taarifa kuu
LIBERIA-WHO-EBOLA-AFYA

Ebola: kesi mpya yathibitishwa Liberia

Kesi mpya ya Ebola imeripotiwa nchini Liberia wakati tarehe 5 Mei nchi hii ilitangazwa rasmi na shrika la Afya Duniani kuwa haina tena virusi vya ugonjwa wa Ebola.

Madaktari wa shirika la Msalaba Mwekundu wakibeba mwili wa mgonjwa aliye fariki, kwa minajili ya mazishi katika mazingira mazuri  ya afya.
Madaktari wa shirika la Msalaba Mwekundu wakibeba mwili wa mgonjwa aliye fariki, kwa minajili ya mazishi katika mazingira mazuri ya afya. AFP PHOTO / ZOOM DOSSO
Matangazo ya kibiashara

Kijana mwenye umri wa miaka 17 alifariki kutokana na virusi vya Ebola wiki mbili zilozopita katika kijiji kinachopatikana mashariki mwa mji mkuu wa Liberia, Monrovia, si mbali na uwanja wa ndege wa kimataifa. WHO imehakikkisha kuwa marehemu alizikwa katika mazingira yaliyo salama.

Kesi hii inatokea miezi miwili baadae shirikia la Afya Duniani kutangaza kwamba Liberia haina tena virusi vya Ebola. Tangazo hili lilitolewa baada ya siku 42 ya mazishi ya mtu wa mwisho aliye ambukizwa virusi vya Ebola, ikiwa ni mara mbili ya kipindi cha kutokomezwa kwa virusi hivyo.

Kesi mpya yaibua maswali

Kesi hii mpya imeibua maswali mengi. Vipi kisa hiki kitaelezwa ? Je, kuna baadhi ya familia ambazo hazikufanyiwa uchunguzi wa virusi vya Ebola ? Je, mgonjwa amesafiri katika nchi jirani ? Hakika, Guinea na Sierra Leone, nchi hizi mbili ambazo zilioathirika na janga hili tangu mwaka mmoja na nusu uliyopita, zimeendelea kukumbwa na virusi vya Ebola tangu mwezi Mei, kutokana hasa na kutoheshimu kanuni za afya.

Hata hivyo viongozi wa afya wa Liberia wamethibitisha kuwa wamekua wakichunguza hasa kwenye maeneo yote alikopita kijana huyo aliye fariki kutokana na virusi vya Ebola.

Kwa upande wake, UNMEER, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa dhidi ya Ebola unaamini kwamba Liberia " bado ipo hatarini kama hatua ya kuudhibiti ugonjwa wa Ebola hadi kufikia kiwango cha sufuri itakua haijaenea katika mikoa yote ya nchi hiyo."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.