rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Burundi Uchaguzi Pierre Nkurunziza Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki Umoja wa Afrika AU

Imechapishwa • Imehaririwa

Shambulio la bomu lajeruhi watu kadhaa Burundi, wakati huu wananchi wakipiga kura

media
Wanajeshi wa Burundi wakilinda usalama kwenye moja ya vituo vya kupigia kura hii leo. AFP PHOTO / MARCO LONGARI

Zoezi la uchaguzi mkuu wa wabunge nchini Burundi limeendelea licha ya shambulio la Guruneti la kurusha kwa mkono kwenye baadhi ya vituo vya kupigia kura, shambulio linalotekelezwa wakati huu upinzani ukiwa umesusia zoezi hili.

 


Vituo vya kupigia kura kwenye baadhi ya maeneo vilichelewa kufunguliwa kutokana na kuchelewa kufika kwa karatasi za kupigia kura pamoja na wafanyakazi.

Watu wasiofahamika wamerisha bomu la kutupa kwa mkono katika baadhi ya vituo jijini Bujumbura na maeneo mengine ya nchi saa chache kabla ya kuanza kwa zoezi la kupiga kura na baada ya kuanza kwa zoezi lenyewe hali ambayo kwa sehemu ilichclewesha kuanza kwa zoezi lenyewe.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametoa wito wa kuahirishwa kwa zoezi la uchaguzi mkuu nchini humo baada ya upinzani kutangaza kuwa hautashiriki uchaguzi wowote unaoandaliwa na Serikali ya rais Nkurunziza.

Akizungumza jijini Bujumbura, naibu mkuu wa polisi, Godefroid Bizimana, amethibitisha kutekelezwa kwa mashambulizi mfululizo ya mabomu ya kurusha kwa mkono, huku akiwanyooshea kidole vijana wa upinzani.

Ulinzi umeimarishwa kwenye vituo vingi vya kupigia kura jijiji Bujumbura na maeneo mengi ya nchi, katika kile polisi inasema ni kuzuia shambulio jingine lolote linaloweza kutekelezwa na makundi ya vijana.

Upinzani nchini Burundi umesusia kushiriki kwenye uchaguzi wa wabunge na ule wa Serikali za mitaaa pamoja na urais kama njia moja wapo ya kupinga hatua ya rais Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu.