Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-UCHAGUZI-USALAMA

Burundi : ”hakuna uchaguzi Ijumaa Juni 5”

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kupitia mshauri wake mkuu wa masuala ya mawasiliano, Willy Nyamitwe, ametangaza kuwa uchaguzi wa Wabunge na Madiwani uliyopangwa kufanyika Ijumaa wiki hii umesogezwa mbele kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu, kama walivyotakiwa na marais wa jumuiya ya Afrika Mashariki Jumapili Mei 31.

Willy Nyamitwe, mshauri mkuu wa rais Pierre Nkurunziza wa masuala ya mawasiliano.
Willy Nyamitwe, mshauri mkuu wa rais Pierre Nkurunziza wa masuala ya mawasiliano. DR
Matangazo ya kibiashara

” Hakuna uchaguzi Ijumaa Juni 5 ”, amesema Willy Nyamitwe, mshauri mkuu wa rais Nkurunziza wa masuala ya mawasiliano.

Hali ya kisiasa na usalama nchini Burundi imeendelea kuwa tete.
Jumapili Mei 31, viongozi wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki walikutana na kuchukua uamzi wa kuitaka serikali ya Burundi na Tume huru ya Uchaguzi (Ceni) kuahirisha kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu uchaguzi huo.

Tume Huru ya Uchaguzi, kwa upande wake, imeendelea kuhakikisha kuwa inaendesha kazi yake kama kawaida licha ya kujiuzulu kwa naibu mwenyekiti wa Tume hiyo, Spes-Caritas Nirondoye, pamoja na mkurugenzi wa masuala ya utawala na fedha, Illuminata Ndabahagamiye. Lakini kujiuzulu kwa watu hao ni tatizo kubwa kwa utendaji kazi wa Tume hiyo ya Uchaguzi.

Hata hivyo tume huru ya Uchaguzi bado inakabiliwa na matatizo ya utendaji kazi, baada ya kujiuzulu kwa wajumbe wake wawili kwa jumla ya wajumbe watano wanaounda Tume hiyo.

Tume huru ya Uchaguzi inapaswa kuchukua maamuzi ya kuandaa uchaguzi kwa makubaliano ya wajumbe wote au kwa idadi kubwa ya wajumbe 4 kwa jumla ya watano wanaounda Ceni.

Kutokana na hali hiyo italazimika kuwateua watu wengine wawili watakaochukua nafasi ya wajumbe hao wawili waliojiuzulu. Na kwa mujibu wa Katiba, inahitaji sheria ya rais baada ya watu hao kupasishwa kwa asilimia 75 ya Wabunge na Maseneta.

Wabunge na Maseneta wameanza kukutana katika vikao mbalimbali tena kuanzia Jumatatu, Juni 1, zikisalia siku 3 za uchaguzi wa wabunge na Madiwani kufanyika kulingana na kalenda ya uchaguzi ya zamani. Hali hii imewashangaza wengi wakati Baraza la Bunge na Seneti vilimaliza muhula wao tangu Aprili 30.

Kinachosalia ni kujua iwapo serikali itafanikiwa kukusanya asilimia 75 za kura kwa kuweza kuwapitisha wagombea hao kwenye nafasi za wajumbe wa Ceni waliojiuzulu, hasa kwa upande wa Baraza la Bunge.

Tume huru ya Uchaguzi iko mbioni kuandaa kalenda ya uchaguzi haraka iwezekanavyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.