rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uturuki IAEA EU

Imechapishwa • Imehaririwa

Kenan Evren aiaga dunia usiku wa leo

media
Jenerali Kenan Evren akiwa makazini kwake mjini Ankara,September 4/ 2010. AFP PHOTO /ADEM ALTAN

Jenerali mmoja aliyehusika katika mapinduzi ya kijeshi yaliyoung'oa uliokuwa utawala wa Uturuki mwaka 1980, Kenan Evren amefariki dunia Jumamosi usiku katika hospitali ya kijeshi katika mji mkuu Ankara, ambapo alikuwa akitibiwa kwa muda wa miaka mitatu.
 


Mamia kwa maelfu ya waturuki hii leo siku ya jumapili wanasema wamesikitishwa na kifo cha kiongozi huyo, aliyewahi kuliogoza taifa hilo kwa muda wa miaka tisa, baada ya kuongoza mapinduzi ya kijeshi mwa 1980.

Evren ameiaga dunia akiwa na umri wa miaka 97.

Bwana Kenan Evren alikuwa Rais wa uturuki mpaka mwaka wa tisa mia themanini na tisa 1989, baada ya kuongoza mapinduzi ya kijeshi ya Septemba 12, 1980.

Inaarifiwa wakati wa mapinduzi hayo, Jenerali Evren alisema mauaji ya washukiwa hayapaswi kuhojiwa, akiongeza kuwa kwani walipaswa kuwalisha magaidi au kuwanyonga.