Pata taarifa kuu
DRC-WANAHARAKATI-USALAMA

DRC: waandishi na wanaharakati wakamatwa

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, viongozi wa mashirika mbalimbali kutoka Burkina Faso, Balai citoyen, na Senegal, Y'en a Marre, wamekamatwa Jumapili alaasiri Machi 15 katika moja ya vitongoji vya mji wa Kinshasa.

Askari polisi, waliotumwa katika mji wa Kinshasa.
Askari polisi, waliotumwa katika mji wa Kinshasa. Naashon Zalk/Bloomberg via Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati hao walikua wakishiriki semina iliyoandaliwa na shirika moja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Filimbi. Uwepo wa wanaharakati hao haukuwafurahisha viongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wanaharakati hao, ambao ni vijana kutoka nchini Burkina Faso, Senegal na Congo, walikuwa na mkutano na waandishi wa habari kuhusu jukwaa jipya la kijamii.

Baada ya mkutano na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya shirika lisilo la kiserikali la Ba jeune Maboko Na Maboko Pona Congo (Tushikamane kwa ajili ya Congo) katika kata ya Masina, Fabel Barro wa shirika la Y'en a marre kutoka Senegal pamoja na Oscibi Johann wa Balai Citoyen kutoka Burkina Faso walikamatwa na polisi. Wanaharakati hao wakiwa pamoja na waandishi wa habari wachache na vijana kadhaa wamekamtwa wakati walipokua wakisubiri tamasha ambalo lingeliandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Filimbi.

Askari polisi wakishirikiana na wanajeshi pamoja na raia waliokua wakivalia nguo za kawaida waliwakamata wanaharakati na waandishi hao wa habari na kuwapeleka hadi kwenye makao makuu ya Idara ya ujasusi (ANR). Wanaharakati wa mashirika ya Y'en a marre na Balai citoyen huenda wakafukuzwa kwenye ardhi ya Congo

Y'en a marre ilichangia kwa kusitisha nia ya Abdoulaye Wade ya kugombea muhula wa tatu nchini Senegal. Kwa upande wake shirika la Balai Citoyen lilihusika katika maandamano yaliyouangusha utawala wa Blaise Compaoré, nchini Burkina Faso.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.