Pata taarifa kuu
RWANDA-KIZITO-SHERIA-HAKI

Kizito Mihigo ahukumiwa kifungo cha miaka kumi jela

Mwanamuziki maarufu nchini Rwanda Kizito Mihigo amehukumia kifungo cha miaka kumi jela. 

Kizito Mihigo mbele ya vyombo vya habari, mjini Kgali Aprili 15 mwaka 2014, siku moja baada ya tangazo la kukamatwa kwake kutolewa.
Kizito Mihigo mbele ya vyombo vya habari, mjini Kgali Aprili 15 mwaka 2014, siku moja baada ya tangazo la kukamatwa kwake kutolewa. AFP PHOTO / STEPHANIE AGLIETTI
Matangazo ya kibiashara

Uamzi katika kesi inayomuhusu Kizito Mihigo na mwandishi wa habari Cassien Ntamuhanga pamoja na watuhumiwa wenzao umetolewa leo Ijumaa Februari 27.

Watuhumiwa hao Wanashtakiwa na serikali ya Rwanda kwa tuhuma za kupanga njama za mauaji, ugaidi na uhaini dhidi ya Serikali ya rais Paul Kagame, kesi ambayo upande wa mashtaka ulitumia mazungumzo binafsi baina ya watuhumiwa hao kwenye intaneti, kama vithibitisho. Utaratibu ambao ulikosolewa vikali hususan na Marekani pamoja na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Shirika la wanahabari wasiokuwa na mipaka (RSF) umekejeli ziara ya rais Paul Kagame aliye alikwa na shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya sayansi na utamaduni Unesco kuhudhuria mkutano kuhusu maendeleo ya teknolojia, wakati Intaneti nchini Rwanda imekua ikidhibitiwa na kukaguliwa na utawala na wakati mwingine kutumika kama chombo cha ukandamizaji.

Kiongozi wa RSF barani Afrika, Clea Kahn-Scriber amesema vyombo vya sheria nchini Rwanda vimekua vikishawiwa na utawala katika kesi mbalimbali, hususan kesi hii inayo muhusu mwanahabari Cassien Ntamuhanga na muimbaji Kizito Mihigo.
Kizito Mihigo kwa mara nyingine alikiri kuhusika na kupanga njama za kuwashambulia viongozi wa kitaifa kwenye serikali inayoongozwa na rais Paul Kagame.

Mihigo aliyasema haya wakati wa ufunguzi wa kesi yake alhamisi Novemba 6 mwaka 2014, ambapo aliwaambia majaji wanaosikiliza kesi yake kuwa kama alivyosema wakati akikamatwa na kuomba msamaha kuhusu tuhuma zinazomkabili, ndivyo anavyosisitiza tena wakati wa kesi yake.

Hivi karibuni wakili wa Mihigo, John Bigaraba alisema kuwa serikali haina ushahidi wowote tosha katika kesi inayomkabili Mihigo na wenzake Jean Paul Dukuzumuremyi ambaye ni mwanajeshi pamoja na waandishi wa habari, Cassien Ntamuhanga na Agnes Niyibizi wameendelea kukanusha mashtaka yao.

Kizito mihigo, ambaye alinusurika katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, alikamatwa Aprili 14 mwaka 2014, wiki moja baada ya familia yake kutojua aliko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.