Pata taarifa kuu
UFARANSA-NIGERIA-NIGER-BOKO HARAM-UGAIDI-USALAMA

Vita dhidi ya Boko Haram, UN yaombwa kuingilia kati

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius, amependekeza kuwa Umoja wa mataifa unapaswa kusaidia kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika dhidi ya Boko Haram.

Laurent Fabius, katika ziara ya kikazi katika ukanda wa Afrika Magharibi, hakusita kutolea wito Umoja wa Mataifa kusaidia kusaidia Umoja wa Afrika katika vita vyake dhidi Boko Haram.
Laurent Fabius, katika ziara ya kikazi katika ukanda wa Afrika Magharibi, hakusita kutolea wito Umoja wa Mataifa kusaidia kusaidia Umoja wa Afrika katika vita vyake dhidi Boko Haram. REUTERS/Adnan Abidi
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Lauren Fabius, ameyasema haya katika ziara yake mwishoni mwa juma hili lililopita katika nchi za Chad, Cameroon na Niger.

Wengi wamekua wakijiuliza kwa nini waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa amependekeza kuwa Umoja wa Mataifa unapaswa kupasisha azimio la kuunga mkono kikosi hiki cha Umoja wa Afrika dhidi ya Boko Haram.

Kwa upande wa Ufaransa, azimio la Umoja wa Mataifa lina faida mbili muhimu. Kwanza, itakuwa ni njia mojawapo ya kusema kwa nchi za Chad, Cameroon, Niger na Benin, ambazo zitaunda kikosi cha kupambana dhidi ya Boko Haram kwamba : "Umoja wa mataifa tunawaunga mkono, lakini wakati huo huo tunawachunguza. Na tutakuwa makini sana na sheria zenu za kujikubalisha ili raia wa kawaida wasiathirike na vitendo vya wanajeshi ambao watakua wamepoteza nidhamu."

" Pia itakuwa ni njia ya kuishawishi Nigeria kurusu kikosi hiki kuingia katika aridhi yake kwa jina ya haki", amesema Laurent Fabius.

Kwa mujibu wa serikali ya Ufaransa, azimio la Umoja wa Mataifa litakipa kikosi hiki uaminifu na nguvu zaidi za kukabiliana dhidi ya Boko Haram. Muhimu zaidi, azimio hilo lingetoa uhalali unaohitajika kwa kuzishawishi nchi tajiri kufadhili vita hivyo dhidi ya Boko Haram.

Lauren Fabius amependekeza kuwa, ingeliwezekana Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lingepitisha azimio hilo mwishoni mwa mwezi Machi, mapema mwezi Aprili. Kisha mkutano wa wafadhili ungelitoa vifaa na kupelekwa kwa wanajeshi katika uwanja wa mapambano. hata hivyo rais wa Niger, Mahamadou Issoufou amesema ili kuondokana na Boko Haram, kuna ulazima jumuiya ya kimataifa ihamasishwe zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.