Pata taarifa kuu
SENEGAL-WADE-HAKI-SHERIA

Karim Wade akabiliwa na kifungo cha miaka 7 jela

Mwendesha mashitaka ameomba kifungo cha miaka 7 jela dhidi ya Karim wade, mwanaye rais wa zamani wa Senegal, Abdoulaye Wade. Ombi hilo la mwendesha mashitaka lilitolewa baada ya miezi 7 kesi inyomuhusu Karim Wade ikisikilizwa.

Karim Wade mbele ya Mahakama inayoshughulikia kesi za kujitajirisha kinyume cha sheria, Machi 15 mwaka 2013.
Karim Wade mbele ya Mahakama inayoshughulikia kesi za kujitajirisha kinyume cha sheria, Machi 15 mwaka 2013. AFP/SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya mashahidi 40 katika keshi hiyo wamesikilizwa, vikiwemo vielelezo na utetezi wa wanasheria wa serikali. Kesi hiyo imemalizika Jumanne wiki hii, na kinachobaki sasa ni uamzi wa majaji.

Karimu, ambaye ni mtoto wa rais wa zamani wa Senegal, anatuhumiwa kujitajirisha kinyume cha sheria na kujihusisha na kashfa za rushwa.

Mwendesha mashitaka , ameomba kifungo cha miaka 7 jela dhidi ya Karimu Wade, pamoja na kulipa faini ya pesa za Senegal bilioni 250 sawa na zaidi ya dola za Kimarekani milioni 200, kunyang'anywa mali na kunyimwa haki za kiraia.

Karim Wade analaumiwa kwa kujipatia zaidi ya dola milioni 200 kwa njia isiyo halali.
Karim Wade anasema kuwa alipata utajiri akiwa mfanyabiashara barani ulaya kabla ya kurejea nyumbani ambapo alihudumu kama waziri kwenye serikali ya babake kwa miaka mitatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.