Pata taarifa kuu
CAR-SELEKA-A-Machafuko-Usalama

CAR: Mapigano yaripotiwa Bria

Mapigano kati ya waasi wa zamani wa Seleka na wanajeshi wa vikosi vya kimataifa yametokea Jumanne asubuhi wiki hii katika mji wa Bria, nchini Jamhuri ya Afrika Kati.

Le quartier Bornou, théâtre des affrontements à Bria en Centrafrique.
Le quartier Bornou, théâtre des affrontements à Bria en Centrafrique. RFI/Hyppolyte Donossio
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya kimataifa vimetangaza kwamba vimeiweka mikononi mwake majengo ya serikali yaliyokua yakishikiliwa na waasi wa zamani wa Seleka

Kwenye saa tano asubuhi magari ya kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa Sangaris wameingia katika mji wa Bria. “ wakazi wa mji huo walishangaa kuona wanajeshi kutoka kikosi Sangaris wakiwasili katika mji huu”, kimeeleza chanzo katika mji huo. Muda mchache baadae mapigano yalizuka katika jengo la serikali lililokua likishikiliwa na wapiganaji wa kundi la waasi wa zamini la Seleka, ambao wanajiita FPRC.

Mapigano hayo yalihusisha wanajeshi wa Ufaransa na wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa mataifa Minusca, upande mmoja na wapiganaji wa kundi la zamani la waasi la Seleka upande mwengine. Hata hivyo magari ya kijeshi ya Ufaransa na helikopta nne vilitumia katika mapigano hayo. Wapiganaji wa kundi la zamani la waasi la Seleka waliamua kurudi nyuma na kuelekea soko kuu, baada ya kuona kuwa wameelewa.

Jumanne mchana wiki hii, milio ya risasi imekua ikisikika katika mji wa Bria, wakati ambapo kikosi cha aUmoja wa Mataifa kilitangaza kwamba “ Minusca ikisaidiwa na wanajeshi wa kikosi cha wanajeshi kutoka Ufaransa wameshikilia baadhi ya majengo ya serikali yakliokua yakishikiliwa na wapiganaji hao wa FPRC”.

Kwa mujibu wa Minusca, operesheni hiyo inalenga la madaraka ya kundi la zamani la Seleka katika ardhi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, na kulindia usalama wa raia. Kundi hio la zamani la Seleka lina wanajeshi wslio kati ya 800 na 1200.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.