Pata taarifa kuu
CAR-ANTIBALAKA-MATEKA-Usalama

Jitihada za askofu Nzapalainga hazijazaa matunda

Wafuasi wa kiongozi wa kundi la Anti-balaka aliekamatwa Jumamosi wiki iliyopita, wanaendelea kumshikilia raia wa Ufaransa, Claudia pamoja na kasisi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambao walitekwa nyara Jumatatu asubuhi.

Askofu mkuu wa Bangui, Dieudonné Nzapalainga.
Askofu mkuu wa Bangui, Dieudonné Nzapalainga. AFP/Steve JORDAN
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo yaliyoanzishwa na askofu mkuu wa Bangui Dieudonné Nzapalainga ili kuwaachilia huru mateka hao hayajazaa matunda.

Haya yakijiri, mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa aliyetekwa nyara Jumanne Januari 20 asubuhi katika mji wa Bangui na watu wenye silaha aameachiwa huru, baada ya siku nzima ya mazungumzo Jumanne wiki hii.

Askofu mkuu wa Bangui, Nzapalainga aliamua kulala nje usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano Januari 21 katika mitaa ya kata ya Boy Rabe, ambapo wanazuiliwa kasisi Gustav na raia wa Ufaransa, Claudia.

Askofu Nzapalainga amechukua uamzi huo ili kuonyesha dhamira yake ya kuhakikisha mateka hao wameachiliwa huru.

Siku nzima ya Jumanne, Askofu mkuu aliendesha mikutano mitatu pamoja na wawakilishi wa kundi la wanamgambo wa Kikristo la Anti-balaka, walioteuliwa na watekaji nyara. Kwa mujibu wa Askofu Nzapalainga, wawakilishi wa watekaji nyara hao, hawakua na hasira kama siku ya kwanza ya mkutano.

Watu hao wamemuahidi Askofu Nzapalainga kwamba huenda mateka hao wakaachiliwa huru leo Jumatano. Hata hivyo Askofu Nzapalainga hajakata tamaa, licha ya kuwa mazungumzo yamemalizika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.