Pata taarifa kuu
RWANDA-DRC-FDLR-ICGLR-IGAD-SADC-Usalama

Mvutano waibuka kuhusu hatua dhidi ya FDLR

Mkutano baina ya Jumuiya ya nchi za ukanda wa maziwa makuu ICGLR na Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za kusini mwa Afrika SADC uliopangwa kufanyika hivi karibuni kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya waasi wa zamani wa Rwanda FDLR umefutwa.

Picha inaonyesha helikopta ya mashambulizi ya MONUSCO, itatoa ulinzi wa angani wakati msafara wa waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR watakaopelekwa katika kambi ya muda ya Kanyabayonga.
Picha inaonyesha helikopta ya mashambulizi ya MONUSCO, itatoa ulinzi wa angani wakati msafara wa waasi wa Kihutu wa Rwanda wa FDLR watakaopelekwa katika kambi ya muda ya Kanyabayonga. Photo MONUSCO/Force
Matangazo ya kibiashara

Awali, mkutano huo uliopangwa kufanyika katikati ya mwezi huu umetangazwa na Waziri wa mambo ya nje wa Angola na kuthibitishwa na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma juma moja lililopita ambapo kufutwa kwake ghafla ili kupisha mchakato wa Umoja wa Mataifa kunazusha hisia tofauti miongoni mwa baadhi ya viongozi wa nchi husika.

Nchi ya Rwanda kupitia Waziri wake wa mambo ya Nje Louise Mushikiwabo imepongeza uamuzi wa nchi ya Angola ambapo Waziri huyo ameandika kwenye akaunti yake ya Twiter kwamba "kwa kweli Rais Dos Santos anajali na kuelewa thamani ya utulivu wa kikanda.

Hata hivyo, zipo pande ambazo zimeelezea kutoridhika kwao ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini ambayo haikuficha ghadhabu yake na kutaka serikali ya Luanda kutoa maelezo, hasa kwa vile Afrika kusini inashutumiwa na Rwanda kutaka kuepuka operesheni ya kijeshi dhidi ya waasi wa FDLR.

Aidha, Tanzania ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya SADC na iliyo na askari wake katika Brigedi ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, inatuhumiwa na seriksli ya Kigali kuwapendelea waasi wa Kihutu wa Rwanda ambapo mwishoni mwa juma lililopita, Waziri wa mambao ya nje wa Tanzania Bernard Membe, amenukuliwa na gazeti la The East African kuwa nchi yake haiko tayari kujikita kwenye opresheni za kijeshi dhidi ya waasi hao ikiwa raia wa kawaida hawatatambuliwa na kulindwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.